UONGOZI WALALAMIKIWA KUUZA ENEO LA KIJIJI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/
Wananchi wa
kitongoji cha Ruvu darajani,wilayani Bagamoyo wamelalamikia hatua ya serikali
ya muda ya kitongoji cha Ruvu kata ya Vigwaza kugawa shamba la kijiji kwa
manufaa binafsi bila kushirikisha wananchi.
Mmoja wa
wananchi hao,BW.ATHUMAN MKALI amesema wamesikitishwa na uongozi wa muda wa
kijiji cha Ruvu kuuza eneo la kijiji bila kushirikisha wananchi,ilihali kuna
wananchi ambao hawana maeneo hata hatua nne kwa ajili ya makazi na mashamba.
BW.MKALI
amebainisha kuwa eneo hilo ambalo ni takriban ekari 10, limetolewa kwa
mwekezaji huyo kinyemela na inasemekana limeuzwa kwa shilingi milioni 50 kwa
mwekezaji, nay eye kuwaahidi kuwajengea vyumba vya zahanati yenye thamani ya
shilingi milioni 25 jambo ambalo wananchi hawakubaliani nayo.
Naye
BW.HEMED IDD ameelezea kuchukizwa na hatua ya uongozi wa muda kuuza eneo la
kijiji kwa faida binafsi, na tukio hilo likiwa linajirudia mara ya pili,
ikilifuatia tukio kama hilo ambapo uongozi uliotolewa awali ulifanya kosa kama
hilo.
Bw.IDD amefafanua
kuwa jambo hilo likifumbiwa macho linaweza kusababisha uvinjifu wa amani
kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi kunakofanywa na uongozi huo wa
muda na bila hatua madhubuti kuchukuliwa kukubaliana na hali hiyo.
Mwandishi wa
habari akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo BW.AHMED KIPOZI kuhusiana na
suala hilo iwapo kama analifahamu, amejibu kwa upande wake yeye hajui uwepo wa
mgogoro huo ila atawasiliana na Katibu tarafa wa eneo hilo kujua
kinachoendelea.END
Comments
Post a Comment