WAKULIMA WALALAMIKIA HATUA YA MKUU WA MKOA
Mgogoro
wa ardhi uliokuwa unafukuta kwa kipindi kirefu kati yaUshirika wa kilimo cha
umwagiliaji Kitomondo na uongozi wa kijiji hicho umeazimia kuitisha kikao cha
wananchama wote kujua hatma ya shamba hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwenyekiti wa wakulima hao,BW.EDWIN MUTAYOBA amesema wao
walifika k atika Bonde hilo ikiwa ni sehemu
ya mkakati kuendesha ukulima wa kisasa.
BW.MUTAYOBA
amedai lakini muda mfupi baada ya wakulima hao kuanza kuliweka shamba hilo katika
mpangilio kwa kuingiza greda katika kuhakikisha mashamba yote yanakuwa na miundombinu
ya barabara likufanya usafirishaji wa mazao kuwa rahisi.
BW.MUTAYOBA
anabainisha baada ya Mkuu wa Mkoa aliyeondolewa BI.AMINA MRISHO ndio alipoamuru
uendelezaji wa shamba hilo ukome na kupelekwa kwa shauri mahakamani kwa madai ya
shamba kutolewa kwa kinyume cha taratibu.
Hata
hivyo baada ya kesi hiyo kufika mahakamani, wakulima wa ushirika huo takriban
600 walifanikiwa kushinda kesi hiyo, lakini kilichojitokeza kwa sasa ni upandishaji
wa ada mbalimbali ili kuwakomoa wakulima.
Na
kwa kuliona hilo wakulima hao 600 wanatarajiwa kukutana Jumamosi , ili kujadili jinsi gani wataweza kuendelea na
kilimo Kwenye Bonde hilo.
END.
Comments
Post a Comment