TUME YATAKIWA KUHARAKISHA UCHUNGUZI
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Chama cha ushirika wa umwagiliaji Bonde la Mto Ruvu mkoa wa
Pwani wilayani Bagamoyo wameitaka tume ya uchunguzi iliyoundwa na naibu waziri
wa kilimo na chakula kufanya uchunguzi huo kwa haraka ili kuweza kupata kiasi
halisi cha fedha zilizopotea.
Maombi hayo yametolewa kwa Mwakilishi kutoka wizara ya
Kilimo na Chakula, BW.HUMPHREY NAMASITE alipokutana na wakulima wa ushirika
huo, kujua hatima ya mgogoro unaoendelea katika ushirika huo.
Ambapo Mwanachama wa ushirika huo SADALLA IDD CHACHA amemuomba
mwakilishi NAMASITE kutoka wizarani kuwaletea matokeo ya tume hiyo iliyoundwa
na Waziri badala ya kuanza kuhoji upya wanachama, kwa kufanya hivyo hatua
madhubuti zinachelewa kuchukuliwa.
BW.HUMPHREY NAMASITE kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula
amewaeleza wanachama wa ushirika huo kuwa wao kama tume iliyoundwa kuchunguza
upotevu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Bodi
iliyovunjwa na Waziri ZAMBI.
Zaidi jionee mwenyewe……..
Comments
Post a Comment