MAADHIMISHO YA WIKI YA WANAWAKE
Ben
Komba,Pwani-Tanzania/12-9-2014/11:15
Katika
kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake nchini, Umoja wa wanawake
Tanzania wilaya ya Bagamoyo umetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
katika kituo cha afya Chalinze mkoa wa Pwani.
Msafara huo
wa kinamama hao ukiongozwa na Mwenyekiti wa UWT wilayani Bagamoyo, BI.HAFSA
KILINDO na Katibu wa Jumuiya hiyo wilayani Bagamoyo BI.TABU HUSSSEIN
walitembelea wadi ya wazazi na nyinginezo na kuwatakiaa uponaji wa haraka.
Akiongea
katika mkutano wa ndani na wanachama wa UWT,Katibu wa wake wilaya ya Bagamoyo,
BI.TABU HUSSEIN amewataka kinamama kuhakikisha wanaandaa mazingira mazuri kwa
watoto wa kike waliomaliza darasa la saba ili waweze kuendelea na masomo ya
ngazi inayofuata.
BI.HUSSEIN
ameongeza ni wajibu wa wanawake kuwalinda watoto wao wa kike na majaribu
mbalimbali na hivyo ni vyema kuwasaidia kishauri ikiwa na kubadil;I mitazamo
tuliyozoea kijamii, jambo ambalo wengine wakiambiwa wanasema wamedharauliwa ili
hali ni ukweli bayana unaofaa kuzingatiwa.
Zaidi
amebainisha katika ukanda wa Pwani watu wanaona fahari kutunzana ngomani badala
ya kupeleka watoto shule na amewasisitiza kuwa wakati umefika kutumia fedha
ambazo wantunzana katika ngoma kuwekeza katika elimu.
END.
Comments
Post a Comment