MWEKEZAJI APIGWA STOP RUVU DARAJANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Wakazi wa Ruvu
Darajani wilayani Bagamoyo kwa kauli moja wameamua kumsimamisha mwekezaji
kuendeleza eneo ambalo inadaiwa amelipata kinyume cha taratibu.
Uamuzi huo umefikia
baada ya kufanyika mkutano wa kijiji kujadili ugawaji holela wa ardhi na
kusimamiwa na mtendaji wa Kata ya Vigwaza BW.MASKUZI MASKUZI ambaye kwa upande
alikiri kuwa makosa yamefanyika katika utoaji wa ardhi katika eneo hilo ambalo
wananchi wanalalamikia.
BW.MASKUZI alitoa
fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu hatua gani zichukuliwe katika
kuhakikisha suala hilo linatatuliwa kwa haraka bila kuleta uvunjifu wa amani
katika kijiji cha Ruvu Darajani kama hali inavyojionyesha kwa sasa.
Wananchi wakichangia
kuhusu suala hilo, BW.ATHUMAN MKALI alikumbushia ujio wa Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, BW.AHMED KIPOZI wakati wa mkutano wa kuondoa uongozi uliopita
kutokana matatizo ya ardhi ambapo alionya uongozi wa mpito usiguse kabisa
masuala ya ardhi mpaka hapo utakapopatikana uongozi kamilifu.
Naye Mwananchi
mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana amependekeza kwa mwekezaji huyo
asimamishwe kuendeleza eneo hilo baada ya yeye kushindwa kutimiza makubaliano
ambayo aliyoahidiana na wananchi huku yeye akitumia fursa hiyo kuingiza mamia
ya ng'ombe kutoka kusikojulikana, hali ambayo wananchi hawakubaliani nayo.
END.
Comments
Post a Comment