WADAU WA ELIMU WALALAMIKA UBORA WA KITABU




WADAU WA ELIMU WALALAMIKA UBORA WA KITABU

Ben Komba/Kibaha- Pwani/15 September 2014
Sept 16

WADAU wa elimu mkoani Pwani wamemlalamikia mchapishaji na msambazaji
wa vitabu vya somo la Advance Level Biology kwa ajili ya kidato cha sita
kinachochapishwa na mkazi aliyetajwa kwa jina la jina tunalo (Fred
Unga) kwa madai ya kukosa sifa za kuchapisha vitini hivyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari mjini Kibaha mkoani Pwani mmoja wa
wadau hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Godfrey alisema kwamba
vitini hivyo vinavyochapishwa na mkazi huyo ambaye ana elimu ya kidato
cha nne ni sawa na kupotosha wanafunzi wenye elimu ya kidato cha sita.

Alisema kuwa wamefuatilia matoleo yanayotolewa na mkazi huyo kisha
kugundua hayana ubora wa kuwawezesha wanafunzi walengwa kuweza kufaulu
vema kwenye masomo yao.


Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mwalimu Mkuu wa Kibiti High School
Wenceleslaus Kihongosi ambaye alisema mtu huyo alisoma shuleni hapo
lakini hakuwahi kufanya mtihani wake wa kidato cha sita baada ya
kufeli somo la chemia kwenye mtihani wa moko hali iliyomsababishia
kuwa na aibu kutokana na kujigamba kulifahamu vilivyo somo hilo.

Uchunguzi zaidi umebaini kwamba mkazi huyo amefoji cheti cha kidato
cha sita  0119/0549 kinachoonyesha alimaliza elimu hiyo Kibaha mwaka
2003 na kupata A ya chemia, B ya biology, C ya Agriculture, S ya
General Study (GS) na S ya basic applied mathematics (BAM) ambacho
amekuwa akitumia kwenda nacho shule mbalimbali kuwarubuni wanafunzi
washawishike kununua vitabu hivyo pamoja na kusoma masomo ya ziada
wakati wa likizo.

mwandishi wa habari hizi alikwenda shule ya sekondari ya Minaki na kuonana na
mwalimu wa taaluma Asha Masonzo ambaye alieleza kuwa vitini vyake
anavisoma japo walimu wa somo hilo wanadai havina ubora.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa Minaki Shukra Yakiti amedai kuwa
ni kweli matilio yake japo mazuri au ya kutegemea sana lakini
wanayasoma na kuyanunua kwa mawakala wake kwani mchapishaji alifika
shuleni hapo na mara moja tena usiku na kuwaeleza alimaliza Kibaha na
kupata A ya chemia na akadai anafundisha masomo ya ziada Ilala Boma
jijini Dar es Salaam kwenye senta yake iitwayo Dar es Salaam Education
Center.

Kwa upande wake mlalamikiwa alipotafutwa kuzungumzia hilo amesema yeye kwa sasa yupo safarini na anatarajia kurejea baada ya wiki tatu ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA