WAHIMZWA KUCHANGAMKIA UJASIRIAMALI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/11:19
Wakulima na
wafugaji nchini wametakiwa kuzingatia kutumia mbinu mpya za kufanya shughuli
zao ili kuwezesha kwa wakati huohuo kutunza mazingira na utunzaji wa uoto wa asili.
Mwakilishi wa
mkuu wa wilaya ya Kibaha, Afisa Tarafa wa Kibaha, BW.ANATOLY MHANGO amesema
kuwa wafugaji wamekuwa wakikata majani mengi kwa ajili ya kulishia mifugo yao
na kutumia kiasi kidogo cha majani kama asilimia 20 na asilimia 80 iliyobaki
yanatupwa.
Bw. MHANGO
ameshauri wafugaji kukata majani ya kulishia mifugo kwa kadri ya mahitaji na
kuyakata kata katika vipande vidogovidogo na kuyatia chumvi, kwa kufanya hivyo
mifugo watakula malisho yao bila kusaza na huku majani mengine yakiwa kama
akiba.
Amewaasa wazee
kujiunga na mafunzo ya mifugo na kilimo ili waweze kutumia muda wao kwa
manufaa, badala ya kukalia kucheza bao na kurandaranda mitaani bila madhumuni
yaliyo bayana.
Naye mkufunzi
wa mafunzo ya ufugaji na kilimo, BW.MHEGELELE MDUDA amesema Chuo chao kimekuwa
kikitoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji ili kuwawezesha wazee na wastaafu
kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuweza kujikwamua kiuchumi.
BW.MDUDA
amesema mafunzo hayo yenye lengo la utajirisho wa ufagaji nyuki, ufugaji samaki
na kilimo yatawawezesha wastaafu na watu wazima katika kufanya shughuli za mali
ambazo zitawawezesha kujikimu hali ngumu ya maisha.
END.
Comments
Post a Comment