WITO WATOLEWA KUSAIDIA YATIMA.

WATOTO YATIMA TUWASAIDIE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-08-2013/10:02

Katika kuhakikisha jamii inawajali watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magummu, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji mdogo wa Bagamoyo BW.ABDUL SHARRIF amezindua rasmi mfuko wao, katika kata ya Miono  wilayani Bagamoyo.

Mwenyekiti huyo wa halmashauri BW.ABDUL SHARRIF ameitaka jamii kulipa kipaumbele suala la watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwapatia nafuu ya kupata baadhi ya mahitaji muhimu.

Amebainisha kuwa yeye mwenyewe ametokea katika uyatima na anajua adha na machungu mbalimbali wanavyokumbana navyo watoto yatima katika maisha ya kila siku na kutokana na hilo akautaka uongozi wa Kata kuanzisha mfuko ambao utasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

BW. SHARRIF kwa kuanzia alitoa shilingi laki tano kwa ajili ya ufunguzi wa akaunti ya mfuko huo wa kuwasaidia watoto yatima na akaahidi na mara baada ya akaunti hiyo kuanza kufanya kazi atawawekea shilingi milioni mbili ili kutunisha mfuko huo.

Katika hafla hiyo fupi Mwenyekiti huyo wa halmashauri ya mji wa Bagamoyo BW. ABDUL SHARRIF alipata fursa ya kula na watoto yatima hao na kuzungumza nao juu ya mambo mbalimbali yanayowasibu katika maisha yao ya kila siku.

Awali kabla ya kula chakula cha mchana na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, BW. SHARIFF aliendesha harambee ya haraka haraka na kufanikiwa kupata jumla ya shilingi milioni 2.3 kama ahadi ikiwa ni mchango kutoka katika vijiji vilivyopo katika Kata ya Miono.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA