SIMBA WAJIPANGA PWANI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-8-2013/12:p30
Wanachama na washabiki wa SIMBA SPORTS CLUB katika Tarafa ya Miono wilaya ya Bagamoyo wameazimia kuanzisha Timu ya mpira wa miguu ambayo itakuwa tanurui la kuoka wachezaji kwa ajili ya kucheza timu ya wakubwa ya Simba katika suala zima la kuibua vipaji.
 
Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mkubwa dawa lililopo mjini Bagamoyo, ABDUL SHARRIF amewaambia wana Simba wakati umefika kwa kutambua kuwa mpira ni ajira na si kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo.
 
SHARRIF amebainisha kuwa Timu hiyo itakuwa chini ya MWALIMU. MTORO MAGOSO ambaye zamani amewahi kuichezea Simba, na kwa kuanzia ametoa nafasi kwa yoyote anayejua anaweza kusakata kabumbu kujitokeza ili kumpa nafasi Kocha kuweza kupata wachezaji stahili.
 
Ameitaka klabu hiyo kutosajili wachezaji kwa kufuata jina au uzuri ili kuepusha uwepo kwa mamluki katika timu hiyo kama ilivyotokea kwa mchezaji MRISHO NGASSA, amesema mpaka sasa tawi la Mkubwa Dawa limeshatoa wachezaji watano ambao wamekwenda Simba B.
 
Aidha alichukua fursa hiyto kukabidhi seti mbili za jezi kwa ajili ya timu hiyo na amewahakikishia wachezaji watakaochaguliwa watapatiwa vifaa kamili vya mazoezi ikiwa pamoja na viatu.
 
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA