BARAZA LA KATIBA LA VIJANA KUFANYIKA KIBAHA

BARAZA LA VIJANA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14:01/22-08-2013
Shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE-YPC- limeandaa mkutano wa Baraza la katiba la vijana wa wilaya ya Kibaha utakaofanyika kwa siku mbili na kuhudhuriwa na vijana 100.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, BW.ISRAEL ILUNDE amebainisha kuwa vijana watakaoshiriki ni pamoja na mabalozi wa YPC KUTOKA KATIKA Kata za halmashauri ya wilaya ya Kibaha, wanachama wa YPC kupitia vikundi vya wanawake vijana (WAVUMA) na wajumbe wa jukwaa la vijana Kibaha,KIBAHA YOUTH FORUM.
Washiriki wengine wawakilishi vijana kutoka kwenye vikundi vya dini pamoja na asasi zingine za vijana na wadau wake,

BW.ILUNDE amefafanua kuwa baraza hilo na vijana na wadau wataweza kutoa maoni yao, wakiwezeshwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, BW.DEUS KIBAMBA.

Mkurugenzi huyo wa YPC, BW.ILUNDE amesema baraza hilo limeandaliwa kisheria chini ya kifungu cha 18(6) cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura ya 83 ambacho kinasemekana “Tume inaweza kuruhusu asasi, Taasisi na Makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni yao juu rasimu ya katiba.

Shirika la lisilo la kiserikali la YPC asasi ya ushirikiano wa maendeleo ya vijana ambayo pia inajihusisha na maendeleo ya jumuiya za kiraia na kijamii kwa ujumla, kwa kuwajengea uwezo kwenye masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kupitia mafunzo na mijadala.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA