WASAIDIWA MAFRIJI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/26-08-2013/17:59
Mbunge wa
Jimbo la Kibaha mjini BW.SYLVESTER KOKA amewasaidia vijana wafanyabiashara wa
stendi ya mabasi ya Mailimoja mjini Kibaha, mafriji mawili yenye thamani ya
shilingi Milioni 1.5.
Akikabidhi mafriji
hayo kwa vijana hao, BW.KOKA amesema ametoa mafriji hayo kwa lengo la
kuwajengea uwezo vijana hao ambao wanajihusisha na kuuza maji ili waweze kupiga
hatua katika biashara zao.
BW.KOKA
amesisitiza lengo ni kuhakikisha uchumi wa wananchi wa Kibaha mjini wanakuwa
wana uchumi utakaowasaidia kupata ustawi wa kimaendeleo na amewakumbusha wana
Kibaha kuhusiana na kauli aliyotoa wakati wa kampeni kuwa atawasaidia wananchi
wote watakaounda vikundi.
Amebainisha kupitia
serikali ya CCM mpaka sasa wameshafanya mambo mengi ikiwamo uimarishaji wa
miundombinu ya barabara na kuimarisha upatikanaji wa maji katika mji wa Kibaha.
Mbunge huyo
wa Kibaha mjini BW.SYLVESTER KOKA amewakumbusha juu ya kabla ya yeye kuwa
mbunge katika kipindi cha mwaka 2010 kulikuwa hakuna hata barabara moja ya lami
lakini kwa sasa mji wa Kibaha ishaanza kujivunia maendeleo yanayotokana na
juhudi za CCM nay eye kama mwakilishi wa wananchi wa Kibaha mjini.
END
Comments
Post a Comment