HIFADHI MSITU RUVU KUSINI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/07-08-2013
Uharibifu wa
hifadhi ya msitu Ruvu Kusini umepungua kufuatia doria kali za mara kwa mara zinazofanywa
na idara ya Maliasili na utalii katika kuhakikisha wanazuaia ukataji wa miti
holela unaotishia kuzuka kwa jangwa.
Hivi
Karibuni mwandishi wa habari hizi amejionea mwenyewe uharibifu unaofanywa na
watu wanaojishughulisha na ukataji wa mkaa kinyume na taratibu na hivyo
kutishia uoto wa asili wa hifadhi hiyo ya Ruvu Kusini.
Mratibu wa
mradi wa mama misitu unaonuia kulinda hifadhi yam situ wa Ruvu Kusini TFC,
BW.YAHYA MTONDA amebainisha katika hatua
ambazo inabidi kuchukuliwa iwapo mtu atakutwa anakata mkaa bila kufuata
taratibu ni kuporwa kwa baiskeli yake ambayo itabidi kulipa faini ili kuipata.
Ameongeza kuwa
kwa mtu yoyote anayekamatwa katika hifadhi anakabiliwa faini ya shilingi elfu
sabini na aidha atawajibika kukilipa kijiji faini ya shilingi elfu 14 na hivyo
kufanya jumla ya faini atakayolipa mtu aliyekiuka taratibu ni sh.elfu 84.
Naye afisa
misitu BW. MHANDO MUBARE amesema kwa sasa msitu huo ndio kwanza unaanza kurudi
katika hali yake ya awali ambapo sehemu kubwa ulibaki mbuga zisizo na miti
kutokana na uoto wa asili kuharibiwa na wakata mkaa na mbao.
BW.MHANDO
amefafanua lakini toka walipoanza kuishirikisha jamii katika kulinda hifadhi yam
situ wa Ruvu Kusini hali imebadilika kabisa, na kwa sasa wanafikiria kutoa
ajira za kudumu kwa watu wanaoshirikiana nao kulinda hifadhi yam situ wa Ruvu
Kusini.
END.
Comments
Post a Comment