AKAMATWA AKIBAKA MPWAWE.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/20-08-2013/10:25
Mkazi mmoja
wa mjini Kibaha eneo la Mailimoja ,BW.SEBASTIAN MAGANGA amethibitika kukamatwa
kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi mtoto wa mdogo wake.
Mwandishi wa
habari hizi ameshuhudia Mkaazi huyo akiwa ameongozana na kundi la watu ilihali
akiwa mwili mzima umejaa damu akiwa na masikitiko makubwa kutokana na aibu.
Kwa mujibu
wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Pwani, Kamishna msaidizi ULRICH MATEI amebainisha
kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mailimoja A, ambapo mtuhumiwa huyo ambaye ana
mke alikuwa na desturi ya kuamka alfajiri kwenda kwa shangazi yake ambaye
wakati huo uwa machinjioni na kumuingilia kimwili binti wa miaka 12 ambaye ni
mwanae.
Kutokana na
kuwa na mazoea hayo ndipo siku ilipowadia aliponasa katika mtego uliotegwa na
shangazi yake mtuhumiwa BIBI. CECILIA MABULA kutokana nay eye kupata taarifa
hizo kuhusiana na mwenendo wa kushangaza wa BW.SEBASTIAN MAGANGA mabaye pia
alikuwa Katibu mwenezi wa CCM kata ya Mailimoja.
END.
Comments
Post a Comment