KIFAA CHA KISASA CHA KUPIMA MWENDOKASI CHAWASILI.
WAENDESHA MAGARI KWA FUJO KUPATIKANA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-08-2013/13:00
Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limeanza majaribio rasmi ya kutumia kifaa cha kupima mwendo kasi kwa magari yanayotumia Barabara ya Morogoro ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara na kusababisha vifo na majeruhi.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani katika mkoa wa Pwani, Mrakibu msaidizi wa NASSORO SISIWAYA amesema kifaa hicho ambacho kitakuwa kinatumia teknolojia ya kisasa itaweza kupunguza malalamiko yanayotolewa na madereva mara wanapokamatwa kutokana na kuendesha gari kwa mwendo kasi.
Mrakibu msaidizi SISIWAYA amefafanua kutoka na kuja kwa kifaa hicho kipya cha kupima mwendokasi wa gari kinachotumia teknolojia ya kisasa na kinachotegemea kwa kiasi kikubwa mtandao wa intaneti ili kufanya kazi kwa usahihi.
Ambapo kwa sasa askari wa usalama barabarani watapunguziwa adha ya kuanza kubisha na madereva wanaoendesha gari kwa fujo, kutokana na kifaa hicho kuwa na uwezo wa kupiga picha na kutunza taarifa ikiwa pamoja na kuonyesha namba za gari inayohusika na hivyo kurahisisha kwa kiasi kikubwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Naye mwakilishi wa kampuni inayosambaza vifaa hivyo amesema wao kwa kushirikiana na wadau kutoka Afrika kusini TMT wanajaribu kuonyesha ubora wa vifaa hivyo katika suala zima la kushirikiana na serikali kuhusiana na kupunguza ajali zinazosababishwa na mwendokasi.
END.

Comments
Post a Comment