FUTARI YATOLEWA KWA WAUMINI PWANI
Ben
Komba/Pwani-TANZANIA/06-08-2013/13:27
Meya mji wa
Bagamoyo ABDUL SHARIF amewataka Waislamu nchini kushirikiana na watu wenye
imani tofauti katika kulijengea Taifa ustawi na kuimarisha umoja na mshikamano
miongoni mwa Watanzania.
BW.SHARIFU
amesema hayo akitoa futari kwa wakazi wa eneo la Miono wilayani Bagamoyo mkoa
wa Pwani, amefafanua kuwa kumekuwa kuna wakijitokeza kujaribu kuanzisha
migogoro ya kidini nchi mwetu ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania, hivyo
amewasihi Waislam kutokubaliana na uchonganishi huo unaotishia ustawi wa jamii
na Taifa kwa ujumla.
Amelaani
baadhi ya wanasiasa wanaotumia mgongo wa dini kwa kujaribu kuanzisha vurugu
nchini kwa lengo la kutaka kuendelea kutawala ilihali toka zamani wakristo na
waislamu wote ni wa moja na wote ni watanzania.
Naye Mbunge
wa Kibaha mjini BW.SYLYVESTER KOKA naye ametoa futari kwa viongozi wa misikiti
56 iliyopo Kibaha ikiwa sehemu ya mchango wake kwa waumini wa dini ya kiislamu
katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
BW.KOKA
alichukua fursa hiyo kuwashukuru Waislamu kwa kumchagua bila kujali kabila lake
wala dini yake, ili hali kuna waislamu wengi mjini Kibaha lakini kwa moyo mmoja
wamempigia kura na hatimaye kuwa mbunge.
Amewaomba
waumini wa dini zote kuheshimiana ili kujenga utangamano na umoja miongoni mwa
watanzania, na kuepusha vurugu za kiimani zinazotokea maeneo mbalimbali nchini.
Naye SHEKHE
SAID LIPAMBILA ,shekhe mkuu wa mkoa wa Pwani
BAKWATA amemshukuru Mbunge huyo kwa kuikumbuka jumuiya ya Kiislam katika
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu
ampe mafanikio na amani.
END.
Comments
Post a Comment