Skip to main content

MEYA SHARRIF AKEMEA UCHUKUAJI WA SHERIA MIKONONI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-8-2013/12:00
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduz wilayani Bagamoyo, BW.ABDUL SHARIFF amewasaidia wakazi wa Mbwewe, Bagamoyo ambao nyumba zao sita zimechomwa moto kufuatia kutokea ajali ya gari eneo hilo na baadhi ya wakazi kukimbilia na kuiba mali zilizokuwamo kwenye gari.
BW.SHARRIF ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya wananchi kuchukua sheria mikononi bila kuhusisha vyombo vya dola, amebainisha kuwa ameshuhudia nyumba hizo zilizochomwa moto na kusikitishwa na hali aliyokuta kutokana katika moja ya nyumba hizo kulikuwa na mgonjwa.
BW.SHARRIF ameshangazwa na Polisi kuwashikilia wanakijiji 5 kwa kosa la kuiba mali katika gari lililopata ajali na wale waliochoma moto wakiachiwa huru na kutokana hali hiyo Mwenyekiti wa wazazi huyo ameahidi kufika eneo hilo siku ya Jumatatu katika kujua ukweli juu ya jambo hilo.
Ameongeza kwa upande wake hafurahishwi na vitendo vyovyote vya uhalifu lakini wananchi hawana budi kufuata taratibu za kisheria katika kukabiliana na uhalifu wowote, na hasa ikizingatiwa nchi yetu haijafikia hatua ya watu kupuuza taratibu za sheria.
BW. ABDUL SHARRIF ameelezea hatua yake ya kutoa usaidizi wa takriban shilingi 1000,000/= kuwasaidia wananchi hao kujenga nyumba za kwa kadiri zilivyokuwa kutokana na wakazi wa nyumba hizo kwa hivi sasa kulazimika kulala nje kutokana nyumba zao walizokuwa kuchomwa moto.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA