KOREA YASAIDIA KITUO CHA AFYA MKOANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12:34/06-08-2013
Kituo cha
afya mkoani katika halmashauri ya mji wa Kibaha kimepata msaada wa fedha zaidi
ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya ya mama na mtoto
katika suala zima la kupunguza vifo vya watoto na kinamama wakati wa
kujifungua.
Akikabidhi
hundi hiyo kwa Mganga mkuu wa mji wa Kibaha, BW.ISSA KANIKI, Balozi wa Korea
nchini Tanzania BW.CHUNG LI amesema kuwa wameshawishika kutoa msaada huo
kupitia shirika la misaada la Korea KOFIH, Ili kusaidia juhudi za serikali
kupunguza vifo vya mama na watoto nchini.
Balozi CHUNG
LI amebainisha kuwa wao kwa upande wao wanapendelea kuona Tanzania inajitegemea
katika suala la afya ya mama na motto ili kujenga Taifa lenye ustawi,
ameyaseama kufuatia swali lililoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na
serikali yao itaendelea kusaidia Tanzania mpaka lini.
Balozi CHUNG
nchi yao imetoa kipaumbele kikubwa katika uimarishaji wa afya ya mama na mtoto
ili kwenda sambamba na malengo ya millennia.
Naye Msimamizi
wa kituo cha Mkoani, BI.JULIETH SANGA ameelezea kufurahishwa kwake na msaada
uliotolewa na KOFIH, kwani utawawezesha kutoa huduma stahili kwa kinamama na
watoto na hivyo kupunguza vifo vya lazima wakati na baada ya uzazi.
BIBI. SANGA
amesema kuwa kwa kupata kiasi hicho cha fedha kutasaidia kwa kiasi kikubwa
kiwango cha utoaji huduma na kuichukulia zawadi hiyo kama msaada mkubwa wa
maendeleo ya mama na motto.
END
heigO � 1 % � ' �'( bsp;
Naye SHEKHE
SAID LIPAMBILA ,shekhe mkuu wa mkoa wa Pwani
BAKWATA amemshukuru Mbunge huyo kwa kuikumbuka jumuiya ya Kiislam katika
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu
ampe mafanikio na amani.
END.
Comments
Post a Comment