MWENGE WA UHURU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10:55/30-08-2013.
Mwenge wa uhuru umemaliza mbio zake katika wilaya ya Kibaha kwa kukagua
na kuzindua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 ikiwa sehemu
ya shughuli zilizofanywa na mbio wilayani Kibaha.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA akiwakabidhi wakimbiza
mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe BIBI. FATMA KIMARIO,
amebainisha kuwa miradi 11 imezinduliwa na kuweka jiwe la msingi katika
wilaya ya Kibaha.
BIBI.KIHEMBA amebainisha kati ya fedha hizo
milioni 73 ni mchango wa halmashauri, milioni 49 mchango wa wananchi
mchango wa wananchi, shilingi milioni 35 mchango wa wadau wengine,
shilingi shilingi bilioni 1.5 ikiwa mchango wa serikali kuu.
Mbio hizo zinaendelea katika wilaya ya Kisarawe ambapo huko unatarajia
kukagua na kuweka mawe ya msingi kwa miradi mbalimbali thamani ya
shilingi bilioni 1.4.
Kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu ni TUSIKUBALI KUBAGULIWA KWA ITIKADI YA AINA YOYOTE, RANGI, DINI WALA KABILA.
END.
Comments
Post a Comment