WAFUGAJI NA WAKULIMA WAVUTANA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/27-08-2013/09:50
Wakulima wa
katika Bonde la mto Ruvu katika kijiji cha Kidogozelo kata ya Vigwaza Tarafa ya
Msoga wameitaka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuwasaidia katika suala zima
la kupambana na wafugaji wanaolisha katika mashamba yao na kuchoma moto vibanda
vya shamba.
Mkazi wa
kijiji cha wakulima cha Kidogozelo BW. OMAR NDEKIO amesema kuwa wakulima
wamekuwa wa desturi ya kuswagia mifugo yao katika mashamba ya wakulima kwa
makusudi na inapotokea mkulima kulalamika wanamtishia.
BW.NDEKIO
amesema agost 22 mwaka huu Shamba lake la nyanya na mahindi lilivamiwa na ng’ombe
na kuharibu kabisa mazao yake kwenye shamba, na kutokana na hilo alichukua
hatua ya kwenda kuripoti Polisi Vigwaza ili kuangalia jinsi gani anaweza
kufidiwa.
Nikiongea na
Mtendaji wa kijiji cha Wakulima cha Kidogozelo, BW.MANENO BUNA amesema yeye
anayo taarifa kuhusiana na uvamizi uliofanywa katika shamba la BW. OMAR NDEKIO.
Na mwandishi
wa habari hizi alipotaka kujua ni hatua gani serikali ya kijiji inachukua hatua
gani kukabiliana na hali hiyo, BW.BUNA amesema kwa sasa mipango inafanyika
kuwepo kwa kikao cha pamoja kati ya wakulima na wafugaji ili kujaribu kuepusha
uvinjifu wa amani.
BW.BUNA
ameongeza kuwa suala la wakulima na wafugaji ni tatizo kubwa na katika ofisi ya
kata kuna migogoro lukuki kuhusiana na migogoro ya wakulima na wafugaji,
wafugaji hao ambao sio wakazi wa maeneo hayo wamekuwa kero tosha kwa wananchi
wa kijiji hicho.
END
Comments
Post a Comment