VUTA NIKUVUTE CDM/CCM PWANI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/14:23/17/7/2013.
cha
Demokrasia na maendeleo kimelalamikia hatua ya viongozi wa halmashauri kuwazuia
kujenga matawi ya chama hicho katika lengo zima la kutekeleza ilani ya chama
chao.
Diwani wa
Kata ya Tumbi, BW. MBENA MAKALA amesema hayo kufuatia vuta nikuvute kati yao na
watu wanaodaiwa kutumwa na wakubwa kusitisha ujenzi wa tawi lao ikiwa sehemu ya
utekelezaji wa kazi zao za siasa.
Bw. MAKALA
amebainisha kuwa imekuwa vigumu kwao wanapotaka kujenga matawi ya chama cha
chao kwa madai ya kuwa wanahitajika kuwa na vibali vinavyowaruhusu kujenga.
Ambapo
BW.MAKALA amebainisha kuwa imekuwa tofauti na wenzao wa chama tawala ambao
wamekuwa wakijenga mashina ya wakereketwa na matawi bila kusumbuliwa na vyombo
vya dola, na kuichukulia hali hiyo kama ukandamizaji wa demokrasia nchini.
Diwani huyo
alishangazwa na diwani wa CCM kata ya Mailimoja BW.ANDREW LUGANO kujaribu kusimamisha ujenzi wa tawi hilo kwa
madai ya kutekeleza maagizo kutoka kwa wakubwa.
Na wananchi
walipotaka kujua ameagizwa na mkubwa gani hakumtaja, hata hivyo mwandishi wa
habari hizi amefanikiwa kuongea na diwani huyo wa Kata ya Mailimoja kutaka
kujua mtu aliyemuagiza kusimamisha ujenzi huo na kudai ni mkurugenzi wa
halmashauri ya mji wa Kibaha.
Juhudi za
kuwasiliana Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha,BI.JENIFA OMOLO
zilishindikana kwa sababu alikuwa kwenye kikao na mkuu wa wilaya ya Kibaha.
END.
Comments
Post a Comment