ABIRIA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO SUMATRA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/7/2013,10:36
Mamlaka ya
ya usafiri wa majini baharini na nchikavu imewataka abiria kushirikiana kwa
karibu na malamka inapotokea ukiukaji wa taratibu za usafiri unaofanywa na
wamiliki na wafanyakazi wa magari ya abiria.
Akiongea na
mwandishi wa habari hizi afisa mfawidhi mkuu wa SUMATRA Mkoa wa Pwani,
BW.NASHON IROGA amesema kumekuwepo na matatizo makubwa wanayokabiliana nayo
katika kuhakikisha huduma za usafiri zinazotolewa zinakuwa katika kiwango
stahili.
BW.IROGA
amesikitishwa na baadhi ya abiria ambao wamekuwa wanashirikiana na wafanyakazi
wa magari ya abiria kukiuka kwa makusudi taratibu za usafiri salama na hata
kushirikiana nao inapotokea bai limeshikiliwa kutokana kukiuka taratibu kwa
kisingizio cha kutaka kufika wanapokwenda.
Naye msafiri
alikuwa anasafiri na na Basi la Mbazi aliyejulikana kwa jina la YUDA kwa upande
wake amesikitishwa na kitendo cha nauli kupandishwa kiholela kwa abiria huku
mamlaka husika zikiwa hazichukui hatua stahili kukabiliana na hali hiyo.
Lakini
katika tukio hilo mwandishi wa habari hizi alishuhudia baadhi ya abiria ambao
walizidishiwa nauli wakirudishiwa fedha zao chini ya usumamizi wa SUMATRA Mkoa
wa Pwani.
END.
Comments
Post a Comment