WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUCHANGIA JAMII.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09:46/09/07/2013.
Wawekezaji
na wafanyabiashara wakubwa nchini wameshauriwa kuwa na utamaduni wa kusaidia
taasisi mbalimbali za kijamii katika suala zima la kuaharakisha maendeleo ya
nchi na wananchi wenyewe.
Hayo
yamezungumzwa na mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini, BW.SYLVESTER KOKA wakati
akikabidhi msaada wa madawati 50 kwa shule za msingi Jitihada na Lulanzi
yaliyotolewa na taasisi ya mikopo kwa wafanyakazi wa umma FAIDIKA.
BW.KOKA
amesema kwa jinsi anavyofahamu uwepo wa wafanyabiashara wenye fedha nyingi
ambao wangefuata nyayo za Taasisi ya FAIDIKA wangeweza kusukuma mbele gurudumu
la maendeleo.
Amebainisha kwa
sasa nchi yetu ina wafanyabiashara mbalimbali wakubwa ambao kama wangekuwa
wanatoa asilimia hata 5 ya walicho nacho katika kuchangia shughuli za kijamii
basa kero nyingi za kijamii zingepungua hususan upande wa elimu.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa taasisi ya mikopo ya FAIDIKA, BW.HARUN FERUZ amesema taasisi
yake imekuwa na utamaduni wa kuchangia madawati katika maeneo mbali yenye
uhitaji ili kuweza kupunguza kero hiyo.
BW. FERUZI
ameongeza kuwa kabla ya kutoa madawati hayo, wanafanya utafiti katika shule
husika kubaini mahitaji halisi ya madawati na wamekuwa wakitoa kwa kadri ya
uwezo wao kutokana na ukosefu wa madawati mashuleni kuwa mgumu.
Akishukuru
kwa kupokea madawati hayo Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lulanzi aliishukuru
Taasisi ya mikopo ya FAIDIKA kwa kuweza kutoa mchango huo na kuwataka wafadhili
wengine kujitokeza kusaidia shule zenye ukosefu mkubwa wa madawati.
END.
Comments
Post a Comment