WANANCHI WATAKIWA KUACHA SHAMBA LA MWENYEWE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, July 18, 2013

Mkuu wa wilaya ya Kibaha BI.HALIMA KIHEMBA amewataka wakazi ambao wanasemekana kuvamia eneo la BW. MOHAMED SUMA kuondoka mara moja ili kutoa fursa kwa mmiliki kuliendeleza.

Akiongea na wakazi wa Mtakuja katika kata ya Pangani halmashauri ya mji wa Kibaha BI.KIHEMBA ambaye ameshafika katika eneo hilo mara tatu katika suala zima la kujaribu kutafuta suluhu kati ya mmiliki na wakazi ambao wanasemekana wamevamia.

BI.KIHEMBA akisoma barua iliyotoka kwa kwa mmiliki wa shamba hilo, BW.MOHAMED SUMA ambayo imefafanua kuhusiana na watu ambao yeye amewakabidhi eneo la heka 16 kwa watu wanane kila mmoja heka 2.

Kwa hatua hiyo BI.KIHEMBA amewasihi wakazi hao kuondoka katika eneo hilo toka wanaokaa eneo hilo wanadai wamepewa bure hivyo amewataka nao kurudisha eneo hillo bure ili kuondoa usumbufu kwa ofisi yake.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtakuja BW. LONGINO KASONTA amesema mzigo mkubwa anasukumiziwa yeye ilihali ambay amesababisha mtafaruku huo aliyekuwa mtendaji kata ya Pangani, BW.JAMES NOYA akiwa haguswi  kabisa.

BW.KASONTA amebainisha kuwa mmiliki wa eneo hilo lenye heka 108, aliridhia binafsi kuto heka 16 kwa baadhi ya wananchi, Lakini bila kutoza fedha zozote, mambo yakabadilika mara baada ya mtendaji wa Kata kuhamishiwa hapo ambapo alianza kugawa eneo hilo kwa ada ya sh.20,000/=, kitu ambacho kilikuwa kinyume na matakwa ya mmiliki.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA