MSASA POLISI JAMII.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013
Wananchi wametakiwa kutumiaulinzi shirikishi jamii kujiletea amani na utulivu katika maeneo kunakosababishwa na watu wanaoishi nao mtaani kwa kutoa taarifa katika suala zima la kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mjini Kibaha, Mrakibu wa Polisi BAKARI KAWINGA amesema hayo wakati alipokutana na polisi jamii katika kata ya Pangani ambapo amefurahishwa kwa Kata hiyo kuwa na matukio kidogo ya uhalifu, kulinganisha na kabla ulinzi huo haujanzishwa.

BW.KAWINGA amebainisha kuwa iwapo umebahatika kuwa Polisi jamii, basi ni vyema kutumia fursa hiyo katika kutenda haki bila kubugudhi wengine kwa kisingizio cha kuwa na namba za simu za wakuu wa Jeshi hilo wa Mkoa wa Pwani.

BW.KAWINGA ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lina nia njema ya kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na wananchi ambao watakuwa na wajibu wa kutoa taarifa wanapoona kuna jambo la kutia mashaka katika mitaa yao.

Aidha amewashauri Polisi Jamii badala ya kila tatizo kulipeleka Kituo cha Polisi wanafursa ya kuwatumia maafisa watendaji wa kijiji na kata kutatua mgogoro wowote kabla ya kuamua kukimbilia Polisi ambako kuna wagharimu wahusika muda na mali kutokana ufuatiliaji wa kesi.

Naye Mratibu Mratibu wa Polisi jamii mkoa wa Pwani, INSPEKTA.ATHUMAN MTASHA amewaambia wlinzi shirikishi hao kuwa wana wajibu wa kuelewa kuwa jukumu la ulinzi ni la kila mmoja wetu ili mradi awe Mtanzania mzalendo mwenye machungu na nchi yake.

INSPEKTA MTASHA ameitaka jamii kujiepusha kuwahukumu Polisi wote kuwa ni wala rushwa au vinginevyo, kwani kila Polisi ana makuzi yake kulingana hulka na tabia za asili za mtu ,na hivyo ingekuwa vyema kutowaweka Polisi wote kwenye kapu moja, kwani kila mtu ana tabia zake.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA