BONANZA LA MICHEZO KWA WANAWAKE KKKT.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:06
Wanawake wakristo
nchini wamehimizwa kushiriki Bonanza la michezo
kwa wanawake wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambayo itakuwa
inafanyika kila baada ya klipindi Fulani katika viwanja vya shirika la elimu
Kibaha.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo, BIBI. VERONICA KILEO amesema kuwa ni
mara yao ya kwanza kuandaa bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha kinamama
washiriki michezo.
BIBI.KILEO amefafanua
kuwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo ina kanda za kiusharika sita ndio
zilizotakiwa kushiriki mashindano hayo lakini hata hivyo ni kanda nne tu
zilizoshiriki Bonanza hilo, na kanda mbili za Zanzibar na magharibi zikishindwa
kufika kutokana na sababu mbalimbali.
BIBI.KILEO
ameongeza kuwa michezo mbalimbali imeshindaniwa katika bonanza hilo ikiwa
pamoja na mazoezi kupasha mwili moto (warmup) kwa takriban dakika 15,kukimbiza
kuku, kuvuta kamba na mpira wa pete.
Mshauri wa
kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo Mama ANNA BAYI amesema hatua hiyo ambayo
wameifikia ni nzuri katika suala zima la kuimarisha michezo upande wa kinamama.
Mama BAYI
anaamini kuwa huo ni mwanzo tu, na anategemea mabonanza mengine yatakuwa bora
zaidi kwani watatumia fursa hii kutambua mapungufu na kurekebisha upungufu huo
ili kuweza kuhamasisha wanawake zaidi
kujitokeza kushiriki.
END.
Comments
Post a Comment