KABURI LABAKI WAZI KULIKOSABABISHWA NA UTAPELI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/31/6/2013/09:45
Katika kile
kinachoashiria kuwa heshima na utu wa mwanadamu unaporomoka kwa kasi, Mtanzania
mmoja anayejulikana kwa jina la ABDUL RAMADHAN amefanya vitendo vya kitapeli
kwa jamii ya waislamu wanaoishi katika maeneo ya Kibaha kwa Mathias mjini
Kibaha.
Inasemekana
kuwa siku ya Jumapili BW.ABDUL RAMADHAN alifika maeneo ulipo msikitini kwa
lengo la kutaka usaidizi wa kumzika mtu ambaye alikuwa mfanyakazi wake wa
nyumbani ambaye amefariki.
BW.RAMADHAN
alimwambia Imamu SAID OMAR wa msikiti QADIRIYA kuwa yeye alikuwa anaishi na
marehemu kama mfanyakazi wa nyumbani lakini kwa bahati mbaya mauti yamemkuta na
hivyo angehitaji msaada wao ili kuweza kwenda kumsitiri marehemu.
Baada ya
kumsikiliza kwa makini Tapeli huyo ambaye uso wake ulionyesha kila dalili za
masikitiko na uchungu usio kifani alipatiwa msaada ambao aliutaka ikiwa pamoja
na wachimba kaburi ambao walifanya kazi yao kwa ufasaha.
Ndipo wakati
ukafika akamwambia Imam OMAR wa msikiti wa QADIRIYA kuwa itakuwa vyema kama
wataenda Mochwari kwa ajili ya kuandaa mwili kwa ajili ya maziko kwa pamoja
akiwemo na mpiga picha waliingia kwenye Taxi kuelekea mochwari.
Wakiwa njiani
ABDUL RAMADHAN alimuomba simu ya mkononi Imam Yule aliyekuwa naye kwa madai ya
kuwa simu yake imekata chaji, bila wasiwasi Imam akamkabidhi simu yake tapeli Yule,
na bado wakiwa njiani tapeli Yule alimuomba mpiga picha kamera yake aangalie
ambapo aliisifia kuwa ni nzuri na kutaka kuinunua.
Mara kabla
hawajafika mochwari ya hospitali ya Tumbi, BW.ABDUL RAMADHAN alishauri ingekuwa
vyema iwapo kwanza wangeenda kununua nyama kwa ajili ya chakula cha msibani, na
kuelekea maeneo ya Mailimoja kwenye bucha ambapo aliagiza kilo 25, wakiwa
pamoja na mpiga picha.
Baada ya
kuzuga kwa muda kidogo tapeli Yule alimuaga mpiga picha kuwa anaenda kununua
viungo vingine kama limao, nyanya na vitunguu kwa ajili ya mboga, ndipo
alipokula kubwa mpaka muda huu.
Kutokana na
hali hiyo mpaka ilipofika saa 12 jioni kulikuwa na kaburi wazi pasi marehemu wa
kuzikwa akiwa hayupo, kutokana na utapeli wabinadamu wenye kupenda kutumikia
njia ya mkato kufanikisha mambo.
END.
Comments
Post a Comment