MADHARA YA MITANDAO
Ben Komba/13:30/19/07/2013.
Matumizi ya mtandao yamekuja na changamoto zake ambazo
zimesababisha kasi mpya ya mmonyoko wa maadili katika jamii, kutokana na baadhi
ya watu kutumia mitandao hiyo kinyume na taratibu zinazongatia ustaarabu na
maadili.
Katika tukio moja mwanadada TAUSI SHAABAN mkazi wa mjini
Kibaha amejikuta katika wakati mgumu kufuatia rafiki yake ambaye amesoma nae
shule ya msingi kumchafua kupitia mtandao wa kijamii PEPERONITY.
Bint. SHAABAN amesema kijana huyo ambaye amefanya hivyo
anamkumbuka kwa jina moja la BARAKA ambaye kwa sasa anaishi Mwanza ambaye kwa
mara ya mwisho alikutana naye Kituo cha Mabasi ya mkoani Ubungo ambapo kijana
huyo alimuomba namba yake ya simu.
Na wakati wakibadilishana namba hizo, Kijana alimuuliza Bint.
Shaaban kama ameshazaa na alipojibiwa ndipo alipoaanza kumwambia maneno ya
kuudhi na kejeli na kumuahidi kuwa atamkomesha, na ndipo jana ghafla akaanza
kupokea simu kutoka kwa wanaume wakware.
Bint. Shaaban ameongeza kuwa mara akaanza kupokea simu kutoka
kwa watu mbalimbali wakitaka kukutana nae kwa lengo la kufanya nao mapenzi kama
alivyojitangaza na kuweka namba yake ya simu ya PEPERONITY ili watakaomhitaji
wampigie.
Amefafanua kuwa alipowauliza wamepata wapi namba yake ya
simu, alijibiwa wameipata katika mtandao huo wa PEPERONITY ambao
unajishughulisha na mambo yanayohusiana na ngono kwa kiasi kikubwa, na hivyo
kuwa na wakati mgumu kutokana muda wote kupigiwa simu na watu wenye mahitaji ya
ngono.
Kutokana na hali hiyo, BINT. TAUSI SHAABAN aliamua kwenda
kituo kidogo cha Polisi Mailimoja mjini Kibaha na kutoa maelezo na huku juhudi
zikifanyika kumtafua anayehusika na udhalilishaji huo wa kijinsia.
Baadhi ya watu niliongea nao kuhusiana na kadhia hiyo,
BW.JOHN GAGARIN ameishauri jamii kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa badala
ya kuchafuana na uhalifu kwa faida ya taifa na jamii kwa ujumla.
Naye Kessy GABRIEL mkazi wa Maili moja mjini Kibaha ameitaka
TCRA kupambana na vitendo vyote vya matumizi yasiyofaa ya mtandao ili kuepusha
usumbufu kwa raia wema unaosababishwa na baadhi ya watu wenye itikadi hasi.
END.
Comments
Post a Comment