ZAO LA UYOGA MKOMBOZI KWA WAJASIRIAMLIA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/13:21/25-07-2013
Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwekeza katika zao la uyoga ili waweze kujiongezea kipato, katika suala zima la kukabiliana na maskini miongoni mwa jamii.

Akiongea katika mafunzo yanayohusiana na kilimo cha zao la uyoga, Mtaalam PETRO MATHEW amebainisha kuwa iwapo wajasiriamli wakiamua kujikita katika kilimo cha zao wataweza kufaidika kiafya na kiuchumi.

BW.MATTHEW amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapatia mbinu na utaalamu wa kufanikisha uoteshaji wa uyoga katika mazingira ya nchi ya Tanzania, ambapo pia uzalishaji wake unasaidia kuweka mazingira katika hali safi, kutokana na kilimo chake kutumia zaidi takataka.

Mtaalamu huyo BW.MATTHEW ameongeza kuwa uyoga ustawi katika takataka ambazo hazijaoza,takataka zilizooza kidogo na hata takataka zilizooza kabisa na hivyo kusababisha matumizi ya takataka kuchukua nafasi kubwa katika uzalishaji wa zao hilo.

BW.MATTHEW ameelezea faida za uyoga ni pamoja na kuongeza kinga za mwili kwa mtumiaji, kupambana na shinikizo la damu, kisukari, vimbe zote ikiwa pamoja na kansa na vitambi visivyokuwa na mpangilio.

Aidha amesisitiza iwapo kilimo cha uyoga kikizingatiwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa familia, ingawa kinakabiliwa na adui mkubwa ambaye ni Panya ambao nao wanaweza kudhibitiwa kwa kuwaoteshea uyoga wa sumu.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA