SKAUTI WAAPISHWA KIBAHA.

MASKAUTI ST.DON BOSCHO WAAPISHWA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:36

Maskauti nchini wametakiwa kuenenda na maisha ya uskauti katika kipindi cha maisha yao yote ili waweze kuishi maisha ya ukakamavu utii na unyenyekevu ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.

Ameyaongea hayo Padri.FULGENCE RUTATEKURURWA wakati wa uapishaji wa maskauti kutoka shule ya ST.DON BOSCHO mjini Kibaha na kuhudhiriwa na maskauti wenzao kutoka nchini USWISSI.

PADRI.RUTATEKURURWA amewataka maskauti hao kuishi maisha ya kiskauti na kuwa changamoto kwa wenzao,ili waweze kujiunga na skauti hivyo ni fursa waliyopewa kama maskauti wapya kuhamasisha wenzao kujiunga nao.

Na amewataka kuambatana na kiapo chao ili waweze kutoa huduma hiyo kwa kufuata kanuni na miongozo ya skauti aidha amewakumbusha mara mtu unapokuwa skauti basi unakuwa skauti milele.

Naye Kamishna msaidizi wa skauti mkoa wa Pwani, Skauta ANTHONY MWENDA  Amesema lengo la hafla hiyo ni kuapisha maskauti wapya wa ST.DON BOSCHO ambao kwa mara kwanza wanaapishwa kuwa skauti.

BW.MWENDA ameongeza kupitia skauti wanatarajia kuwajenga vijana katika hali ya upendo, uzalendo na ukakamavu ili waweze kutumika mara wanapohitajika katika matukio mbali.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA