VIDEO-WANANCHI BAGAMOYO WALALAMIKIA KUSITISHWA KWA MNADA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/26/2015 12:21:34 PM
Wakazi wa
kijiji cha Ruvu Darajani wilaya ya Bagamoyo katika mkoa wa Pwani wamelalamikia
uongozi wa wilaya ya Bagamoyo ya kuzuia kufanyika mnanada katika eneo hilo kila
siku.
Mmoja wa
wafanyabiashara wa ng’ombe ambaye nimebahatika kuongea naye,BW.DEOGRATIUS
KIWALE amesema yeye kama mfanyabiashara wa ng’ombe wamekuwa wakinunua ng’ombe
kutoka maeneo mengine na kuja kuwauza katika mnada huo wa Ruvu.
BW.KIWALE
ameongeza kuwa wao wamekuwa wakilipa kodi mbalimbali ambazo kwa njia moja au
nyingine zimekuwa zimekuwa zinawasaidia wakazi wa kijiji hicho na kijiji
chenyewe katika kuwawezesha kugharimia huduma mbalimbali za kijamii.
Naye mkazi
mwingine wa kijiji cha Ruvu,BW.SADALAH CHACHA amebainisha kuwa hatua ya kusimamisha
mnada ni kuwakomoa wakazi wa Ruvu kutokana na wao kukataa kupokea wavamizi
ambao wamevamia eneo hilo na Mkuu wa wilaya kuamrisha watu hao wapatiwe maeneo
katika eneo lililovamiwa.
BW.SADALAH
amefafanua kuwa mnada huo ni kitega uchumi cha kijiji,halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo na serikali kuu, na hausiki kupokea ng’ombe kutoka nje ya mkoa na kwa upande wao hawakubaliani
na hatua hiyo na amemtaka mkuu wa wilaya kufika kijijini hapo kutafuta ufumbuzi
wa jumla.
Awali
akisoma barua kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, BW.HEMED MAJID MWANGA,
Mtendaji wa kijiji cha Ruvu darajani, BI.RIZIKI MLELA imeagiza kuanzia sasa
mnada huo utakuwa siku moja na kuwataka wananchi kuchagua siku moja ya juma kwa
ajili ya mnada.
END.
Comments
Post a Comment