VIDEO-WAANANCHI WAMTAKA MKUU WA WILAYA BAGAMOYO KUWAFIKIA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/24/2015 11:41:03 AM
Wananchi wa
Ruvu Darajani wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wametamka mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, BW.HEMED MAJID MWANGA kutokaa ofisini na kutoa amri tata bila ya
mwenyewe kujitoa na kufika maeneo yenye migogoro.
Hayo
yamezungumzwa na mwananchi, BW.RAMADHAN KONDO katika mkutano maalum wa kijiji
cha Ruvu darajani kujadili mgogoro unaokisibu kijiji hicho kwa sasa,ambapo
amesema kauli anazotoa mkuu wa wilaya zina utata kutokana nay eye kukaa ofisini
tu badala ya kwenda kuonana na wananchi.
BW.KONDO ameongeza ni vyema sasa kwa Mkuu wa wilaya kutoka badala ya kutegemea kupelekewa taarifa ambazo zina mashaka na ulaghai, kwa yeye kutoa amri tata ni kuvuka mipaka ya wajibu wake na amemtaja mkuu wa wilaya kama ndio chanzo cha mtafaruku huo.
Naye
mwananchi mwingine,BW.RASHID GAMA ameeleza kushangazwa kwamtendaji wa kijiji
RIZIKI MLELA kutokana na mgogoro huo ikiwa ni sehemu ya vitisho kutoka kwa mkuu
wa wilaya.
BW.GAMA
amefafanua kuwa wao kama wananchi hawatakubaliana na hatua hiyo ya mkuu wa
wilaya toka kijiji cha Ruvu Darajani ndicho kimesajiliwa na ameutaka uongozi wa
kijiji kuwaweka wazi watu ambao wamekwenda Polisi waliozusha kwamba kuna vurugu
zinataka kufanywa na wakazi wa Ruvu Darajani.
Mtendaji wa
Kijiji cha Ruvu Darajani, BW.RIZIKI MLELA akisoma barua kutoka kwa mkuu wa
wilaya kwa wananchi ambayo imeelekezwa kwa Mwenyekiti wa kijii cha Ruvu
darajani, ambao imeagiza kwa uongozi wa kijiji kugawa eneo ambalo limevamiwa
kwa wavamizi na kama atapuuza basi atachukua hatua ya kinidhamu.
END.
Comments
Post a Comment