MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ATAKIWA KUTOKA OFISINI NA WANACHI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/24/2015 11:41:03 AM
Wananchi wa Ruvu Darajani wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wametamka mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, BW.HEMED MAJID MWANGA kutokaa ofisini na kutoa amri tata bila ya mwenyewe kujitoa na kufika maeneo yenye migogoro.

Hayo yamezungumzwa na mwananchi, BW.RAMADHAN KONDO katika mkutano maalum wa kijiji cha Ruvu darajani kujadili mgogoro unaokisibu kijiji hicho kwa sasa,ambapo amesema kauli anazotoa mkuu wa wilaya zina utata kutokana nay eye kukaa ofisini tu badala ya kwenda kuonana na wananchi.

BW.KONDO ameongeza ni vyema sasa kwa Mkuu wa wilaya kutoka badala ya kutegemea kupelekewa taarifa ambazo zina mashaka na ulaghai, kwa yeye kutoa amri tata ni kuvuka mipaka ya wajibu wake na amemtaja mkuu wa wilaya kama ndio chanzo cha mtafaruku huo.

Naye mwananchi mwingine,BW.RASHID GAMA ameeleza kushangazwa kwamtendaji wa kijiji RIZIKI MLELA kutokana na mgogoro huo ikiwa ni sehemu ya vitisho kutoka kwa mkuu wa wilaya.

BW.GAMA amefafanua kuwa wao kama wananchi hawatakubaliana na hatua hiyo ya mkuu wa wilaya toka kijiji cha Ruvu Darajani ndicho kimesajiliwa na ameutaka uongozi wa kijiji kuwaweka wazi watu ambao wamekwenda Polisi waliozusha kwamba kuna vurugu zinataka kufanywa na wakazi wa Ruvu Darajani.

Mtendaji wa Kijiji cha Ruvu Darajani, BW.RIZIKI MLELA akisoma barua kutoka kwa mkuu wa wilaya kwa wananchi ambayo imeelekezwa kwa Mwenyekiti wa kijii cha Ruvu darajani, ambao imeagiza kwa uongozi wa kijiji kugawa eneo ambalo limevamiwa kwa wavamizi na kama atapuuza basi atachukua hatua ya kinidhamu.

END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA