MWANDISHI AJITOKEZA UDIWANI MJINI KIBAHA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/17/2015 12:30:16 PM
Mwanahabari
BW.DAVID GAUDENCE MSUYA amejitosa kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya
Tangini mjini Kibaha, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mjini Kibaha,
kufuatiwa na kuombwa na wananchi wa Kata husika.
Akitangaza
azma yake ya kuwania nafasi hiyo, BW.MSUYA amesema kuwa yeye anao uzoefu wa
muda mrefu katika masuala ya siasa na ameguswa na matatizo mbalimbali
yanayowakabili wakazi wa Kata hiyo na hivyo akipewa nafasia atahakikisha
anawasaidia kwa njia moja au nyingine.
BW.DAVID
GAUDENCE MSUYA ambaye ni mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo leo,
amebainisha katika uchunguzi ambao amefanya matatizo mengi yanayowakabilIi
wananchi yapo ndani ya uwezo wao, ingawa pia yapo machache ambayo Halmashauri
nayo inahitajika kutoa usaidizi.
END.
Comments
Post a Comment