MWANAMAMA AJITOKEZA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE KIBAHA VIJIJINI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/26/2015 11:05:45 AM
Vugu Vugu za
uchaguzi zimeanza katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini kwa Mwanamama EDITHA
BABEIYA amejitokeza kugombea ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA katika Jimbo
hilo.
Mwanamama huyo
EDITHA BABEIYA ameeleza sababu kubwa yeye kuamua kugombea nafasi ya Ubunge ni
kiu yake ya kutaka kuwaletea maendeleo wapiga kura wa Kibaha vijijini ambao kwa
muda sasa wameongozwa na wabunge ambao si wakazi.
BI.EDITHA BABEIYA
ameelezea mbinu ambazo atazitumia endapo atabahatika kupata nafasi hiyo ya uwakilishi
ni kuwashirikisha wananchi wote katika utoaji wa maamuzi kuanzia ngazi ya chini
hadi utekelezaji.
Na amewataka
wapiga kura inapofika sehemu yeye ameshinda atafanya kila awezalo kuwaunganisha
wananchi wote bila kujali Itikadi, BI.EDITHA BABEIYA ameshakabidhi fomu hizo
rasmi katika ofisi za Jimbo za CHADEMA Kibaha vijijini sambamba na fomu ya
kugombea ubunge viti maalum.
Comments
Post a Comment