VIJANA WAENDELEA KUJITOKEZA KUTIA NIA UDIWANI KIBAHA-VIDEO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/19/2015 9:29:42 AM

Kuendelea Kujitokeza Kwa Makada Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi katika kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi kumezua ari mpya ya vijana kushiriki msuala ya Siasa.

Mmoja wa kada kijana kabisa kutangaza nia ni BW. CHRISTOPHER ELIAS MJEMA ambaye yeye amejinasibu kutia nia kugombea nafasi ya Udiwani Kata ya Mailimoja A.

Bw .MJEMA amebainisha kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kuangalia kwa karibu matatizo yanayowakabili wananchi ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya uhakika ya mawasiliano  na umeme.

Amefafanua, BW.MJEMA iwapo wananchi wakimpatia nafasi hiyo ya kuwa Diwani wa kwanza wa Kat hiyo mpya, hawatajutia uamuzi wao na akiwachukulia wao kama waajiri wake.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA