MTENDAJI WA KIJIJI ASHIKILIWA KISA UVAMIZI WA ARDHI RUVU DARAJANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/19/2015
3:38:25 PM
Katika hali
isiyo ya kawaida Mtendaji wa Kijiji cha Ruvu darajani amejikuta amewekwa
kizuizini kufuatia wananchi wa kijiji cha Ruvu darajani kutaka kufanya mkutano
kujadili hatua ya baadhi ya wananchi kuvamia eneo la kijiji hicho na kuanzisha
makazi bila kuwashirikisha wananchi.
Mtendaji huyo
wa kijiji cha Ruvu darajani, BI.RIZIKI MLELA ameshikiliwa baada ya kupigiwa
simu kutoka Tarafani muda mfupi kabla ya kuanza mkutano huo wa kijiji ambao
moja ya agenda ni kujadili kauli ambayo inadaiwa kutolewa na Mkuu mpya wa
wilaya ya Bagamoyo, ya kutengua makatazo yote ambayo yametolewa mtangulizi
wake.
Kitendo cha
Mkuu huyo mpya ya wilaya ya Bagamoyo, BW.MAJID MWANGA kimewanyong’onyeza
wananchi wa kijiji hicho ikizingatiwa ardhi iliyopo hata wenyewe haiwatoshi na
itakuwaje yeye mgeni kupuuza wenyeji wake.
Mwanakijiji wa Ruvu darajani, BW.RAMADHAN KONDO amesema
mara baada ya wanakijiji kulalamika juu
ya uwepo wa wavamizi katika kijiji chao ilihali wenyewe hawana hata ardhi, na mkutano
ambao wameuandaa ulikuwa ni wa amani.
Na ameshangazwa
na Mkuu wa wilaya kutoa amri ya kusema wavamizi hao wasibuguziwe kutokana na
wao ni raia wa Tanzania, na kuhoji ukiwa raia unaruhusiwa kuvunja sheria.
Mwenyekiti wa
kijiji cha Ruvu darajani,BW.KAMBONA KWALO ameelezea kushangwaza kwake na
Mtendaji wa Kijiji,BI.RIZIKI MLELA
kuwekwa kizuizini na Katibu tarafa, na hivyo wamechukua hatua ya halmashauri ya
kijiji hicho na baadhi ya wananchi kwenda kujua kilichojiri.END.
Comments
Post a Comment