WAANDISHI KUPATIWA ELIMU YA KODI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/25/2015 11:51:00 AM
Shirika
lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE kwa kushirikiana na
ACTION AID wameandaa mafunzo rasmi ya uelewa juu ya nguvu ya Kodi na
uwajibikaji kupitia mradi wa VIJANA VOICE IN ACCOUNTABILITY(VIVA).
Mkurugenzi
Mtendaji Wa Shirika la YPC, BW.ISRAEL ILUNDE akizungumza na mwandishi wa Habari
hizi ofisini kwake mjini Kibaha, amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo
kwa waandishi wa Habari kufahamu michakato ya maendeleo ya umma ili waweze
kutoa mchango wao katika kufanikisha mradi na kuchochea uwajibikaji kwenye
serikali za mitaa na taifa kwa ujumla.
BW.ILUNDE
ameongeza mbali ya kujenga uwezo kwa waandishi wa Habari mradi huo pia unalenga
kuwapatia elimu na kuwajengea uwezo wa vijana na jamii nzima katika kuchochea
uwajibikaji wa jamii katika kuchochea uwajibikaji katika vijiji,vitongoji na
mitaa,pamoja na taasisi katika suala zima la kuleta maendeleo endelevu nchini.
END.
Comments
Post a Comment