SHERIA KANDAMIZI YAKEMEWA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6/17/2015 12:09:25 PM
Hatua ya
serikali kutunga muswada kandamizi juu ya uhuru wa kujieleza ina lengo la
kuhakikisha watawala wanaendesha mambo watakavyo wenyewe hata kama wakiwa
wanafanya kinyume bila kukosolewa, hali ambayo itachochochea kasi ya ufisadi wa
mali ya umma nchini.
Mwanasheria
DAMAS NDUMBARO ameyasema alipokuwa anatoa mada kwa viongozi vijana wa Afrika
katika ofisi ya Taasisi ya FRIEDRICH EBERT STIFTUNG, ambapo amefafanua sheria
hiyo itawafanya watumiaji waz mtandao kuwa katika mtego wa kushitakiwa muda
wowote.
BW.NDUMBARO
amebainisha kuwa sheria hiyo inaminya uhuru wa kujieleza wa raia ambapo vitisho
na adhabu kali kwa yoyote ambaye atakaiuka masharti magumu yaliyowekwa na
sheria hiyo kandamizi.
BW.NDUMBARO
ameongeza kuwa adhabu ambazo zitatolewa ni kifungo miaka cha miaka mitano jela
au faini ya shilingi milioni 20 kwa mwananchi ambaye atatiwa hatiani na
kuzitaja sheria ya kupata Habari ya mwaka 2015, sheria ya vyombo vya
Habari,sheria ya mtandao na takwimu ni shoka juu ya uhuru wa kujieleza.
Naye
BW,HENRY MUHANIKA mwezeshaji mwandishi
wa Habari nguli, ameishangaa serikali kuleta miswada hiyo katika kipindi hiki
kueleka uchaguzi, kitu ambacho kina lengo la kuwabana wananchi wa kawaida
wasiweze kupata taarifa muhimu na sahihi kuhusu mustakabali wa nchi yao
kisiasa,kijamii na kiutamaduni.
Naye
Mwakilishi wa FREDIRICH EBERT STIFTUNG nchini, BW.ROLF PAASCH amewataka
wanahabari nchini kuacha kujifafanisha na wataalamu wa kada nyingine kama ya udaktari, uanasheria na uhandisi
kwani hakuna uhusiano kabisa na kada hiyo ambayo imejikita kwa mwananchi
mwenyewe kupitia uhuru wa kujieleza.
Ameongeza
kuwa nchini Ujerumani hakuna utaratibu kama huu ambao umependekezwa katika
sheria ya mtandao ya kutaka waandishi wawe wamesajiliwa kitu ambacho ni cha
kushangaza na kinaweza kukiletea taifa matatizo hasa kutokana na uhuru wa
kujieleza kuwa sehemu ya masharti ya Benki ya Dunia kutoa misaada kwa nchi
maskini.
BW.PAASCH
amefafanua kuwa kupitia uhuru wa kujieleza hali ya uwajibikaji na matumizi
sahihi ya fedha za umma utaimarika na hivyo, kuweza kuwabana mafisadi ambao
hawataki mambo mabaya ya kwao kuwekwa wazi.
END.
Comments
Post a Comment