VIDEO-WAZEE WAPAATIWA VITAMBULISHO VYA KUPATIWA TIBA BURE.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/5/14/2015 11:20:28 AM
Jimbo la
uchaguzi Sumbawanga mjini linatarajiwa kuwaka moto katika uchaguzi mkuu ujao
baada ya watia nia mbalimbali kujitokeza kutaka mkupata nafasi ya uwakilishi wa
Jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mheshimiwa AESHI MOHAMED kwa tikiti
ya CCM.
Mmoja wa
waliojitokeza kutia nia kutaka nafasi ya uwakilishi Bungeni ni Mtumishi wa
Idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW.FRANK MWALEMBE ambaye yeye
ni mzaliwa wa manispaa ya mji wa Sumbawanga.
BW.MWALEMBE kabla
ya kujiunga na halmashauri ya mji wa Kibaha kama mtumishi, Alipata elimu yake
katika shule ya msingi Malagano, elimu ya sekondari ya Seminari ya Kahengesa na
“A level” Katika shule ya Pugu High School na baadaye alifanya kazi ya Ualimu
katika shule ya sekondari ya Makuzani na Rukwa high school kwa muda wa mwaka
mmoja na nusu kama Mwalimu wa nidhamu.
Na ilipofika
mwaka 2005-2006, BW.FRANK MWALEMBE alijiunga na chuo kikuu cha ardhi cha Dar es
Saalam na kufanikiwa kupata BACHELOR OF
SCIENCE IN LAND MANAGEMENT AND VALUATION.
Baada ya
kuhitimu aliomba kazi katika halmashauri ya mji wa Kibaha akiwa kama Afisa
ardhi ambapo baada ya miaka miwili alichaguliwa kuwa mfanyakazi bora mwaka 2011
ikiwa pamoja na kupandishwa daraja.
BW.MWALEMBE
amebainisha kuwa lengo kubwa la kutia nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia
Tiketi ya CCM ni kutokana na yeye kuyaelewa vizuri mazingira ya Mkoa wa Rukwa
na maisha ya kijamii pamopja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa
Manispaa ya Sumbawanga mjini.
END
Comments
Post a Comment