VIDEO-VURUGU ZAZUKA MKUTANO WA MBUNGE KIBAHA MJINI.
Ben
Komba/Pwani-Kibaha/5/18/2015 2:40:05 PM
Mkutano wa
hadhara ambao umefanywa na Mbunge wa Kibaha mjini,MH. SILVESTRY KOKA kutokea
kwa vurugu ambazo zimesababisha mtu mmoja kujeruhiwa kutokana na kupita na
bango ambalo liliwakera wana CCM.
Hali hiyo ambayo
iliotewa toka mapema kabla ya mkutano, Baada ya Katibu wa Mbunge huyo,
BW.METHOD MSEMBERE kumnwambia mwandishi wa Habari hizi kuwa kuna kikundi cha
vijana ambacho kimepanga kufanya vurugu katika mkutano mkuu wa mheshimiwa
mbunge.
BW.MSEMBERE
ameongeza kuwa kuna watu wanataka kufanya fujo katika mkutano huo na kutuhumu
moja ya kambi zilizo ndani ya chama hicho ambazo zinawania nafasi ya Bunge.
Na kweli
ilipofika muda wa mkutano baada ya MH.KOKA kumaliza kufungua mashina ya CCM na
kurudi kwa ajili ya mkutano ndipo vijana kadhaa wa CHADEMA walipojitokeza na mabango ambapo moja ya
bango hilo ambalo lilisema TUNASHUKURU MBUNGE WETU KWA KUJA KUTUAGA, BYEBYE, na
ndipo mmoja wa viongozi wa CCM wilaya akachukuwa mabango hayo na kuanza
kulichana.
Ndipo vijana
wa CCM wakaanza kumshambulia mshika bango huyo mpaka Polisi walipomwokoa na
kumweka kituoni.
Baadhi ya
wananchi ambao wanaunga mkono mabango mwanachama wa CHADEMA, BW.FADHILI
NGONYANI amesema kuwa ni haki ya wananchi kushika mabango ili kufikisha ujumbe
wa kero zinazowakabili kwa viongozi wao, na kumtaka mbunge kutambua yeye ni wa
wananchi wote sio CCM pekee.
Katibu
wa ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY
mkoa wa Pwani, NDG.MRISHO KHALIFAN SWAGALA amesikitishwa na utamaduni unaooanza
kujengeka miongoni mwa Watanzania ambao ukiachiwa uendelee utasababisha madhara
makubwa kwa usalama wa nchi.
End.
Comments
Post a Comment