VIASHIRIA VYA VURUGU VYAANZA KUJITOKEZA- KIDEO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/5/25/2015 2:48:06 PM
Viashiria ya kuwepo kwa vurugu katika uchaguzi mkuu ujao imeanza kujitokeza rasmi na hali ikiwa ya wasiwasi kutokana na baadhi ya wanaowania nafasi mbalimbali za uwakilishi wakiandaa vikundi vya vijana wahuni kwa ajili ya kuwatumia kipindi cha uchaguzi mkuu ujao wa Rais, Madiwani na wabunge unaotarajiwa kufanyika hapo Oktoba 25 mwaka huu.

Hivi karibuni katika Mkutano wa hadhara ambao umefanywa na Mbunge wa Kibaha mjini,MH. SILVESTRY KOKA na kutokea kwa vurugu ambazo zimesababisha mtu mmoja kujeruhiwa kutokana na kupita na bango ambalo liliwakera wana CCM.

Hali hiyo ambayo iliotewa toka mapema kabla ya mkutano, Baada ya Katibu wa Mbunge huyo, BW.METHOD MSEMBERE kumwambia mwandishi wa Habari hizi kuwa kuna kikundi cha vijana ambacho kimepanga kufanya vurugu katika mkutano mkuu wa mheshimiwa mbunge.

BW.MSEMBERE ameongeza kuwa kuna watu wanataka kufanya fujo katika mkutano huo na kutuhumu moja ya kambi zilizo ndani ya chama hicho ambazo zinawania nafasi ya Bunge.

Na kweli ilipofika muda wa mkutano baada ya MH.KOKA kumaliza kufungua mashina ya CCM na kurudi kwa ajili ya mkutano ndipo vijana kadhaa wa CHADEMA  walipojitokeza na mabango ambapo moja ya bango hilo ambalo lilisema TUNASHUKURU MBUNGE WETU KWA KUJA KUTUAGA, BYEBYE, na ndipo mmoja wa viongozi wa CCM wilaya akachukuwa mabango hayo na kuanza kulichana.

Hapo vijana wa CCM wakaanza kumshambulia mshika bango huyo mpaka Polisi walipomwokoa na kumweka kituoni.

Baadhi ya wananchi ambao wanaunga mkono mabango mwanachama wa CHADEMA, BW.FADHILI NGONYANI amesema kuwa ni haki ya wananchi kushika mabango ili kufikisha ujumbe wa kero zinazowakabili kwa viongozi wao, na kumtaka mbunge kutambua yeye ni wa wananchi wote sio CCM pekee.

Katibu wa  ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY mkoa wa Pwani, NDG.MRISHO KHALIFAN SWAGALA amesikitishwa na utamaduni unaooanza kujengeka miongoni mwa Watanzania ambao ukiachiwa uendelee utasababisha madhara makubwa kwa usalama wa nchi.

End.




Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA