AJITOKEZA KUTIA NIA UBUNGE SUMBAWANGA MJINI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/5/14/2015 11:20:28 AM
Jimbo la uchaguzi Sumbawanga mjini linatarajiwa kuwaka moto katika uchaguzi mkuu ujao baada ya watia nia mbalimbali kujitokeza kutaka mkupata nafasi ya uwakilishi wa Jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mheshimiwa AESHI MOHAMED kwa tikiti ya CCM.

Mmoja wa waliojitokeza kutia nia kutaka nafasi ya uwakilishi Bungeni ni Mtumishi wa Idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW.FRANK MWALEMBE ambaye yeye ni mzaliwa wa manispaa ya mji wa Sumbawanga.

BW.MWALEMBE kabla ya kujiunga na halmashauri ya mji wa Kibaha kama mtumishi, Alipata elimu yake katika shule ya msingi Malagano, elimu ya sekondari ya Seminari ya Kahengesa na “A level” Katika shule ya Pugu High School na baadaye alifanya kazi ya Ualimu katika shule ya sekondari ya Makuzani na Rukwa high school kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kama Mwalimu wa nidhamu.

Na ilipofika mwaka 2005-2006, BW.FRANK MWALEMBE alijiunga na chuo kikuu cha ardhi cha Dar es Saalam na kufanikiwa  kupata BACHELOR OF SCIENCE IN LAND MANAGEMENT AND VALUATION.

Baada ya kuhitimu aliomba kazi katika halmashauri ya mji wa Kibaha akiwa kama Afisa ardhi ambapo baada ya miaka miwili alichaguliwa kuwa mfanyakazi bora mwaka 2011 ikiwa pamoja na kupandishwa daraja.

BW.MWALEMBE amebainisha kuwa lengo kubwa la kutia nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia Tiketi ya CCM ni kutokana na yeye kuyaelewa vizuri mazingira ya Mkoa wa Rukwa na maisha ya kijamii pamopja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga mjini.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA