TASAF YATUMIA BILIONI.1.6 WILAYANI KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/5/22/2015 10:48:18 AM
Zaidi  ya shilingi Bilioni 1,657102301/= zimetumika na TASAF halmashauri ya wilaya ya Kibaha na kupata mafanikio makubwa katika kuhakikisha jamii maskini zinapata mahitaji stahili ili kujenga jamii ambayo itakuwa na uwezo wa kujikimu na maisha yenye kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi.

Mratibu wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW.GODSON HARRY amesema hayo ofisini kwake akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, ambapo amesema kuwa mpaka sasa kwa upande wa zoezi la uhawilishaji fedha kaya zaidi ya 5000 zimefaidika na mpango huo.

BW.HARRY ameongeza kupitia mpango huo wamefanikiwa kuwatambua na kuwaandikisha walengwa watakaohusika mpango huo wa uhawilishaji wa Fedha kwa kaya maskini, wenye lengo la kuinua uchumi wa jamii maskini zaidi.

Amebainisha toka kuanzishwa kwa mpango mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwa pamoja na ongezeko la uandikishaji wa watoto mashuleni kutoka katika kaya lengwa ikiwa pamoja na kupanda kwa mahudhurio ya wanafunzi mashuleni, kuongezeka kwa ufaulu katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu.

Mratibu huyo wa TASAF amefafanua katika upande wa afya, kupitia elimu waliyotoa na vigezo vinavyozingatiwa vya kuwahimiza kinamama kupeleka watoto kliniki na hivyo kuwepo kwa ongezeko kubwa la watoto ambao wanapelekwa kliniki, sambamba na kuimarika kwa uchangiaji wa mfuko wa Bima ya afya ya jamii.

Aidha, B W.HARRY akizungumzia changamaoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya kaya kushindwa kuandikishwa pamoja na umaskini walionao kwa kushindwa kutoa majibu sahihi kwenye madodoso na wengine kutokuwepo siku ya uandikishaji.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA