TIBA YA BURE KWA WAZEE YAZINDULIWA KIBAHA.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/5/13/2015 10:01:45 AM
Mpango wa Tiba bure kwa wazee wa umri wa miaka 60 na kuendelea umeziinduliwa mjini Kibaha kwa wazee 4672 kupatiwa vitambulisho vya kuwawezesha kupatiwa tiba bure inapotokea kuwa wameugua.

Mganga wa mkuu wa halmashauri ya mji wa Kibaha, DKT.ISSA KANIKI akisoma taarifa maalum kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kibaha, BI.JENIFA CHRISTIAN amesema halmashauri ya mji wa Kibaha katika kutekeleza sera ya Taifa ya wazee, imeamua kuweka suala hilo kwa vitendo.

DKT.KANIKI amebainisha kuwa ambapo halmashauri ilianza kwa kufanya tathimini ya utekelezaji wa sera hiyo,kwa kufanya uhamasishaji katika ngazi ya jamii na kutoa elimu ya ufahamu juu ya uwepo wa mpango huo, Kwa kutumia takwimu ya sensa ya wakazi katika halmashauri ya Mji wa Kibaha aambapo inakadiriwa kuwa na wazee 5,111.

Ameongeza DKT.KANIKI kuwa Jumla ya fedha zilizotumika kutengeneza vitambulisho hivyo 4672 ni shilling milioni 11.7 na amewashukuru ustawi wa jamii na Good Samaritan (HELP AGE) INTERNATIONAL  kwa mchango wao wa hali na mali.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa  Kibaha, BIBI.JENIFA CHRISTIAN  amewataka Wazee watambue kuwa serikali yao inawependa na kuwathamini katika kuhakikisha afya za wazee zinalindwa kwa kufuta taratibu zenye lengo la kuwapunuzia mzigo.

Bibi .CHRISTIAN amesema kilio cha wazee cha kwenda hospitalini na kutotambulika sasa kimepata jibu, kwa wazee kupatiwa vitambulisho ambavyo vitawawezesha  kupata tiba kwa urais kwa kuvivaa vitambulisho wanapofika hospitalini.


END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA