MANIPULATION OF POWER aka ULAFI WA MADARAKA.
▼ππ
ππFriday, May 22, 2015
HABARI KUBWA LEO-VITA MPYAA YAIBUKA,TV ,REDIO NA SERIKALI,DK MENGI ASEMA TBC HAPANA,SOMA HAPA KUJUA
pichani ni Rais Jakaya kikwete picha na Maktaba
SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi CCM ni kama imeiingia kwenye Ugomvi mkubwa na Vyombo Vya Habari Binafsi ikiwemo Redio na TV baada Serikali hiyo kukaribia kupitisha sheria Mbaya zaidi kuwaitokea nchini hususani kwenye Sekta ya Vyombo vya Habari tangu nchini kupata Uhuru.Mtandao huu umeelezwa .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Sheria hiyo ambayo imesukwa kwa ustadi mkubwa kwa shinikizo la Waziri Mmoja Mwandamizi wa Serikali ya Kikwete ni ile inayosema kwamba Vyombo vya Habari Binafsi ikiwemo TV na Redio ifikiapo saa 2 usiku ni lazima wajiunge moja kwa moja na Taarifa za Habari zitakazokuwa zinarushwa na TBC 1 kwa upande wa TV na Tbc Taifa kwa upande wa Redio.
Sheria hiyo ambayo teyari ipo mikononi mwa Bunge inatarajiwa kupitishwa haraka sana kabla ya uchaguzi mkuu unaofanyika hapo baadae mwaka huu kama zilivyoptishwa Sheria mbili ambazo ni ile ya Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Akizungumza kwa Uchungu Wiki hii Jijini Dar es Salaam kuhusu Sheria hiyo inayonyonga na kumaliza Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambapo amesema inashangaza kuona serikali kwa makusudi inataka kuanzisha mgogoro na vyombo vya habari binafsi kwa kupora uhuru wa wananchi kupata habari.
Alisema serikali inapaswa kuangalia kwa umakini ili baadaye pakitokea tatizo la uvunjifu wa amani isije kulaumiwa, kwamba ilikuwa chanzo cha kutokea machafuko kwani amani haiwezi kuwapo bila uhuru.
Dk. Mengi alitolea mfano kifungu cha 14 cha Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari kinachosema “chombo cha habari binafsi kinatakiwa kujiunga na chombo cha habari cha umma kwa ajili ya taarifa za habari kila siku saa mbili usiku ili kuwezesha umma kufuatilia masuala muhimu ya kitaifa."
Alisema kwa maana nyingine, ITV haiwezi kurusha taarifa yake ya habari saa 2:00 usiku kwa kuwa italazimika kujiunga na Televisheni ya Taifa (TBC) na kwamba, hilo linadhihirisha chombo binafsi cha habari hakina ruhusa au uhuru wa kurusha taarifa yake.
“Tunarudi tulikotoka, yaani kwamba hakuna uhuru wa vyombo vya habari binafsi kufanya kazi zake Tanzania.
Ni njia mojawapo ya kuua uhuru wa vyombo binafsi vya habari... sijawahi kuona nchi yoyote ambayo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu serikali ya nchi hiyo inaanzisha migogoro na vyombo binafsi,” alisema na kuongeza:
“Ni matumaini yangu kuwa itafika mahali serikali itaona inachofanya siyo sawa na wanapora wananchi uhuru wa kupata habari... kuna vifungu vingine ni vibaya, havisaidii taaluma ya habari.”
“Uhuru wa vyombo vya habari ndiyo unawapa wananchi nafasi kuwa huru kuzungumza kwa kutoa maoni yao, katika hali ya sasa na ukichukua mapendekezo bungeni, vyombo vya habari vitakosa uhuru, hivyo wananchi watakuwa wamenyang’anywa uhuru wao,” alisema na kuongeza:
“Amani siyo ya mtu mmoja, amani siyo ya chama fulani, amani siyo ya kikundi fulani cha watu na hakuna anayeweza kusema yeye anahodhi amani... amani ni mali yetu wote na kila mtu awe kiongozi au mtu wa kawaida ni lazima ashiriki katika kujenga amani yetu.”
Alisema wakati ukizungumzia amani, huwezi kuacha kuzungumzia uhuru wa vyombo vya habari ambavyo ni muhimu katika kudumisha uhuru wake.
“Mimi napata shida na haiingii akilini mwangu ninapoona serikali kwa makusudi kabisa inaanza migogoro na vyombo binafsi vya habari vyote... katika hilo serikali inakuwa kama inachochea kuwapo na hali ambayo haisaidii vyombo vya habari kuandika juu ya umuhimu wa amani na ninadhani ina sababu zake sizielewi, sijaona nchi yoyote duniani inaanzisha ama inazalisha migogoro na vyombo vya habari miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu,” alisema.
Dk. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, alisema tasnia ya habari imepiga hatua kubwa na kutoa uhuru wa kufikisha habari ambazo ni za kweli na huru kwa wananchi.
“Unapoona pendekezo katika miswada ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari na Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata taarifa ya mwaka 2015, ambayo iko bungeni, unaona ni njia ya kuua vyombo vya habari binafsi,” alisema.
Wasomi wanena
Wakizungumza na Mtandao huu wasomi wa mambo ya Habari pamoja na waandishi wa Habari wamesema ni wazi Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM ikiongozwa na Rais Jakaya kikwete imeshalewa madaraka na inataka kuvuruga Amani ya Nchi.
“Hii serikali isijidanganye na Jeshi lao Polisi kwa kutaka kuipitisha misheria ya kibabe kama hii,leo wanataka kuwalazimisha watanzania waangalia taarifa za Habari za chama cha Mapinduzi zinatorushwa kwenye TV ilijivisha vazi la CCM ya TBC,kwasababu tupo katika Mfumo wa soko huria vyombo vya Habari viwe huru leo TBC imekuwa TV inayoficha maovu makubwa ya Serikali”
Vilevile Wasomo hao wakaenda mbali na kusema ni kama Rais Jakaya Kikwete anataka kumaliza Vibaya kwenye Utawala basi aipitisha sheria hiyo ambapo wanadai zitamfanya wananchi wamchukie.
“Rais kikwete alianza vizuri kwa kutoa uhuru wa Vyombo vya Habari, sasa najua wanataka kutumi wingi wa Wabunge wa CCM kupitisha Sheria za kutesa wananchi kama ile ya Uharifu wa Mitandaoni ambao umewanyonga watanzania ,na sasa wakaoni haitoshi wanataka kupitisha sheria hii ni wazi kiongozi huyo anataka kujichafua akitoka madarakani au wanataka watu hata wakimuona wamteme mate”waliohoji

Comments
Post a Comment