WAHITIMU WAUGUZI 15 WALIOMALIZA MAFUNZO 2012 WA UUGUZI COTC WALILIA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/5/30/2015 10:18 AM
Wanafunzi 15
wa fani ya uuguzi waliomaliza mafunzo yao mwaka 2012 katika chuo cha uuguzi shirika la elimu Kibaha
mpaka sasa hawajapatiwa vyeti vyao vya kuwahalalisha kufanya kazi hiyo na
kuweza kutoa huduma kwa jamii.
Akizungumza na
mwandishi wa Habari hizi katika siku ya kuadhimisha sherehe ya wauuguzi
Ulimwenguni, Muuguzi BW.IBRAHIM MSAFIR amesema kuwa wanaguswa sana kwa wenzao
kuhitimu masomo ya uuguzi na baadaye kutopewa vyeti.
BW.MSAFIR
amebainisha kuwa kila baada ya muda Fulani wizara ya afya inakagua vyuo vyote
vinavyotoa mafunzo ya afya na kuvitambua ambavyo vitakidhi matakwa ya Wizara,
ingawa kwa sasa Chuo chao kinatambulika na kulitaka Shirika la Elimu kukaa kwa
pamoja na wizara ya afya kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wauguzi wenzao.
Naye muuguzi
mkuu, BI.ELIZABETH MLACHA amesema FLORENCE NIGHTANGELE ambaye amezaliwa 12 Mei
1928 na kuamua kujiunga na kazi ya uuguzi ambayo ilikuwa kinyume na matakwa ya
wazazi wake.
BI.MLACHA
ameongeza kuwa ni juu ya wauguzi kutumia utaalam wao kwa manufaa ya jamii
mahali popote alipo kutokana na uuguzi kuwa fani ambayo haina mipaka kama
alivyofanya FLORENCE NIGHTANGELE wakati wa vita kuu ya pili ya dunia ambapo
alijitolea kuwasaidia maaskari majeruhi wa kipindi hicho.
END.
Comments
Post a Comment