VIDEO-WAHITIMU 15 MWAKA 2012 CHUO CHA UUGUZI SHIRIKA LA ELIMU WALILIA VYETI VYAO



Ben Komba/Pwani-Tanzania/5/30/2015 10:18 AM
Wanafunzi 15 wa fani ya uuguzi waliomaliza mafunzo yao mwaka 2012  katika chuo cha uuguzi shirika la elimu Kibaha mpaka sasa hawajapatiwa vyeti vyao vya kuwahalalisha kufanya kazi hiyo na kuweza kutoa huduma kwa jamii.

Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi katika siku ya kuadhimisha sherehe ya wauuguzi Ulimwenguni, Muuguzi BW.IBRAHIM MSAFIR amesema kuwa wanaguswa sana kwa wenzao kuhitimu masomo ya uuguzi na baadaye kutopewa vyeti.

BW.MSAFIR amebainisha kuwa kila baada ya muda Fulani wizara ya afya inakagua vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya afya na kuvitambua ambavyo vitakidhi matakwa ya Wizara, ingawa kwa sasa Chuo chao kinatambulika na kulitaka Shirika la Elimu kukaa kwa pamoja na wizara ya afya kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wauguzi wenzao.
Naye muuguzi mkuu, BI.ELIZABETH MLACHA amesema FLORENCE NIGHTANGELE ambaye amezaliwa 12 Mei 1928 na kuamua kujiunga na kazi ya uuguzi ambayo ilikuwa kinyume na matakwa ya wazazi wake.

BI.MLACHA ameongeza kuwa ni juu ya wauguzi kutumia utaalam wao kwa manufaa ya jamii mahali popote alipo kutokana na uuguzi kuwa fani ambayo haina mipaka kama alivyofanya FLORENCE NIGHTANGELE wakati wa vita kuu ya pili ya dunia ambapo alijitolea kuwasaidia maaskari majeruhi wa kipindi hicho.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA