HATIMAYE VIDEO YA TASAF KUTUMIA SHILINGI BILIONI 1.6 KIBAHA HII HAPA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/5/22/2015 10:48:18 AM
Zaidi ya shilingi Bilioni 1,657102301/= zimetumika
na TASAF halmashauri ya wilaya ya Kibaha na kupata mafanikio makubwa katika
kuhakikisha jamii maskini zinapata mahitaji stahili ili kujenga jamii ambayo
itakuwa na uwezo wa kujikimu na maisha yenye kukabiliwa na changamoto
mbalimbali za kiuchumi.
Mratibu wa
TASAF halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW.GODSON HARRY amesema hayo ofisini
kwake akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, ambapo amesema kuwa mpaka sasa kwa
upande wa zoezi la uhawilishaji fedha kaya zaidi ya 5000 zimefaidika na mpango
huo.
BW.HARRY
ameongeza kupitia mpango huo wamefanikiwa kuwatambua na kuwaandikisha walengwa
watakaohusika mpango huo wa uhawilishaji wa Fedha kwa kaya maskini, wenye lengo
la kuinua uchumi wa jamii maskini zaidi.
Amebainisha
toka kuanzishwa kwa mpango mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwa pamoja na
ongezeko la uandikishaji wa watoto mashuleni kutoka katika kaya lengwa ikiwa
pamoja na kupanda kwa mahudhurio ya wanafunzi mashuleni, kuongezeka kwa ufaulu
katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu.
Mratibu huyo
wa TASAF amefafanua katika upande wa afya, kupitia elimu waliyotoa na vigezo
vinavyozingatiwa vya kuwahimiza kinamama kupeleka watoto kliniki na hivyo
kuwepo kwa ongezeko kubwa la watoto ambao wanapelekwa kliniki, sambamba na
kuimarika kwa uchangiaji wa mfuko wa Bima ya afya ya jamii.
Aidha, B
W.HARRY akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya kaya kushindwa
kuandikishwa pamoja na umaskini walionao kwa kushindwa kutoa majibu sahihi
kwenye madodoso na wengine kutokuwepo siku ya uandikishaji.
END
Comments
Post a Comment