TANESCO YANUIA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA PWANI.
TANESCO PWANI YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Jan-13/08:23:59 Shirika la umeme katika mkoa wa Pwani linatarajia kufikia wateja elfu 17500 kwenye kipindi cha mwaka 2013-2014 ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafiki wateja wengi zaidi katika lengo la kuwafikia wateja 250,000 nchi nzima sawa na kupunguza bei ya uunganishaji wa huduma hiyo kwa wateja. ... Meneja wa TANESCO mkoa wa Pwani, BW. JOHNSON MWIGUNE amesema shirika hilo lina mikakati ya kurekebisha utoaji huduma, kwa kuhakikisha kuna kuwa na ongezeko la wateja wapya ili kuongeza makusanyo ya kila mwezi ya shirika, na katika kuvutia wateja shirika limeanza kwa kushusha bei ya kuunganisha huduma hiyo kwa wateja wa kawaida hali ambayo inatoa fursa kwa watu wenye kipato cha kati kupata huduma hiyo. BW.MWIGUNE amesisitiza kuwa shirika lake litaendelea na zoezi la ufungaji wa mita za luku kwa wateja wake katika suala zima la matumizi ya digitali na kuachana na Mita za analogia na zoezi hilo limefanikiwa kwa asi...