Posts

Showing posts from May, 2016

VIDEO-WAJAWAZITO WASAIDIWA MJINI KIBAHA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/05/2016 13:40:29 Taasisi ya Kimataifa ya Uingereza ya hiyari ya ABUBAKAR DARWESH imetoa msaada kwa akinamama wajawazito wa Kituo cha afya mkoani Mjini Kibaha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu ambao wamejiwekea katika kusaidia jamii zenye mahitaji. Mkurugenzi wa taasisi hiyo BW. BILAL DARWESH akikabidhi msaada bhuo amesema kuwa amevutika kutoa misaada ya kiutu kufuatia safari ambayo amefanya toka Dar es Saalam mpaka Sumbawanga na kushuhudia changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi. Msaada ambao umetolewa na taasisi hiyo ni mabeseni na kila hitaji la mtoto anapozaliwa vikiwa vimefungwa kwa pamoja, aidha ameongeza kuwa Taasisi yake inajishughulisha na usaidizi kwa watu wa imani zote na ikiwa ni moja la lengo kubwa la uanzishaji wake ili kuwawezesha watu wa imani tofauti kuishi pamoja. Naye mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kibaha, DR. HAPPINESS NDOSI ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada ambao wameutoa kwa kina mama wajawazito...

VIDEO-MAANDAMANO YA WAFANYABIASHARA KIBAHA YAZUIWA NA POLISI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26/05/2016 14:34:40 Maandamano ya wafanyabiashara wa soko la Maili moja mjini Kibaha kulalamikia hatua ya halmashauri ya mji kutowajengea soko na ilihali wakitakiwa kuhama eneo ambalo kwa hivi sasa linatumika kabla zoezi la bomoaaboma halijaanza yamenyimwa kibali na Jeshi la Polisi. Maandamano hayo ambayo yangehusisha wafanyabiashara wa soko hilo yalipangwa kuelekea moja kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, kutokana na kutaka kuonana naye kwa kipindi kirefu bila mafanikio. Kwa mujibu wa Katibu wa umoja wa wafanyabiashara sokoni Mailimoja, BW. MUHSIN ABDUL amewaambia wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo kuwa maandamano ambayo walikuwa wayafanye yamesitishwa na Jeshi la Polisi kutokana na kuhofia uvunjifu wa amani ambao ungeweza kujitokeza. Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara hao, BW. ALLY GONZA maarufu kama Mzee wa Shamba, amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu kungojea hatua nyingine am...

POLISI YAZUIA MAANDAMANO YA WAFANYABIASHARA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26/05/2016 14:34:40 Maandamano ya wafanyabiashara wa soko la Maili moja mjini Kibaha kulalamikia hatua ya halmashauri ya mji kutowajengea soko na ilihali wakitakiwa kuhama eneo ambalo kwa hivi sasa linatumika kabla zoezi la bomoaaboma halijaanza yamenyimwa kibali na Jeshi la Polisi. Maandamano hayo ambayo yangehusisha wafanyabiashara wa soko hilo yalipangwa kuelekea moja kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, kutokana na kutaka kuonana naye kwa kipindi kirefu bila mafanikio. Kwa mujibu wa Katibu wa umoja wa wafanyabiashara sokoni Mailimoja, BW. MUHSIN ABDUL amewaambia wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo kuwa maandamano ambayo walikuwa wayafanye yamesitishwa na Jeshi la Polisi kutokana na kuhofia uvunjifu wa amani ambao ungeweza kujitokeza. Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara hao, BW. ALLY GONZA maarufu kama Mzee wa Shamba, amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu kungojea hatua nyingine amba...

VIDEO-KIKONGO WALALAMIKA KUHUJUMIWA MAPATO YAO NA HALMASHAURI YA WILAYA KIBAHA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 10:43:00 Wananchi wa Kata ya Kikongo wamelalamikia halmashauri ya wilaya ya Kibaha kusitisha uchimbaji wa madini ya mchanga ambao ulikuwa unaipatia Kata hiyo mapato na kutoa fursa hiyo kwa mtu binafsi. Mwenyekiti wa zamani wa serikali ya kijii cha Kikongo, BW. JUMA JUYA amesema kuwa akiwa katika hiyo  amesema akiwa mkusanyaji wa fedha za   mchanga ikiwa pamoja na kuwasomea mapato na matumizi na wakawa wanaenda sawa na wananchi. BW.JUYA ameongeza makusanyo ambayo yalikuwa yanapatikana yalitumika katika shughuli mbambali za maendeleo ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya hamsini ambao waliweza kujikimu kimaisha. Naye BW. SALUM SAID amesema kuwa wamestuka kwamba mapato ya kijiji ya yanahujumiwa kutokana na wananchi kuamua kuunda kamati ya muda ya kusimamia shimo hilo ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja wa kamati ya muda iliweza kukusanya takriban shilingi milioni 3.5 na hivyo kuweka wazi mapato ambayo yaliku...

MEI 23 SIKU YA FISTULA ULIMWENGUNI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/22/05/2016 09:53:51 Maadhimisho ya siku ya Fistula ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 23 mwaka huu Mashirika yanapambana na tatizo hilo nchini yamelenga katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari ili kuweza kufikisha elimu juu ya ugonjwa huo kwa jamii. Mwakilizi msidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa UNFPA nchini, BI. CHRISTINE MWANUKUZI KWAYU amesema kwa kushirikiana na vyombo vya habari kutawezesha wanawake wanaoishi na tatizo la Fistula kujitambua na kuchukua hatua sthahili. BI. KWAYU amebainisha kuwa takriban wanawake milioni mbili wanaishi na tatizo hilo ulimwenguni na inakadiriwa wanawake takriban 800 wanafariki dunia kwa tatizo la fistula kwa mwaka. Aidha amefafanua Mwakilishi msaidizi huyo wa UNFPA nchini, BI. KWAYU kuwa athari ambazo zinawapata wagonjwa hao ni pamoja na kunyanyapaliwa na jamii kutokana na hali ya kutokwa haja bila kujitambua. Akizungumzia kuhusiana na kundi ambalo linapata kwa kiasi kikubwa t...

VIDEO=KAYA YA PANGANI MJINI KIBAHA WASAKA DARAJA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 12:15:47 Wakazi wa mtaa wa Mkombozi katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameazimia kujenga daraja litakalounganisha manispaa ya Kinondoni na halmashauri ya mji wa Kibaha ili kupunguza usumbufu unaowapata wananchi wa pande hizo wakati wa mvua. mmoja wa wakazi wa Mtaa huo ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema kuwa wao kama kamati ya ujenzi wa daraja hilo walikagua maeneo yote ambayo wanadhani panafaa kujenga daraja. Ambapo hapo palizuka vuta nkuvute kati ya wajumbe wa kamati hiyo na kila mmoja akipenda eneo tofauti kwa ajili ya ujenzi huo na katika kipindi hicho tayari fedha zaidi ya shilingi milioni mmoja zilikuwa zimeshakusanywa. Walikatishwa tamaa na kauli ya mmoja wa wataalamu wa ujenzi kutoka halmashauri ya mji wa Kibaha ambaye aliwaambia kujenga daraja eneo hilo kungehitaji zaidi ya shilingi bilioni ambapo katika kipindi  hicho hawakuwa nazo fedha hizo. Diwani wa Kata ya Pangani, BW.AGUSTINO MDACHI amewataka wananch...

VIDEO-KIKONGO WILAYA YA KIBAHA WALALAMIKIA HALMASHAURI KUHUJUMU MAPATO YAO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 10:43:00 Wananchi wa Kata ya Kikongo wamelalamikia halmashauri ya wilaya ya Kibaha kusitisha uchimbaji wa madini ya mchanga ambao ulikuwa unaipatia Kata hiyo mapato na kutoa fursa hiyo kwa mtu binafsi. Mwenyekiti wa zamani wa serikali ya kijii cha Kikongo, BW. JUMA JUYA amesema kuwa akiwa katika hiyo  amesema akiwa mkusanyaji wa fedha za   mchanga ikiwa pamoja na kuwasomea mapato na matumizi na wakawa wanaenda sawa na wananchi. BW.JUYA ameongeza makusanyo ambayo yalikuwa yanapatikana yalitumika katika shughuli mbambali za maendeleo ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya hamsini ambao waliweza kujikimu kimaisha. Naye BW. SALUM SAID amesema kuwa wamestuka kwamba mapato ya kijiji ya yanahujumiwa kutokana na wananchi kuamua kuunda kamati ya muda ya kusimamia shimo hilo ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja wa kamati ya muda iliweza kukusanya takriban shilingi milioni 3.5 na hivyo kuweka wazi mapato ambayo yaliku...

WANANCHI WA KATA PANGANI MJINI KIBAHA WASAKA DARAJA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 12:15:47 Wakazi wa mtaa wa Mkombozi katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameazimia kujenga daraja litakalounganisha manispaa ya Kinondoni na halmashauri ya mji wa Kibaha ili kupunguza usumbufu unaowapata wananchi wa pande hizo wakati wa mvua. mmoja wa wakazi wa Mtaa huo ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema kuwa wao kama kamati ya ujenzi wa daraja hilo walikagua maeneo yote ambayo wanadhani panafaa kujenga daraja. Ambapo hapo palizuka vuta nkuvute kati ya wajumbe wa kamati hiyo na kila mmoja akipenda eneo tofauti kwa ajili ya ujenzi huo na katika kipindi hicho tayari fedha zaidi ya shilingi milioni mmoja zilikuwa zimeshakusanywa. Walikatishwa tamaa na kauli ya mmoja wa wataalamu wa ujenzi kutoka halmashauri ya mji wa Kibaha ambaye aliwaambia kujenga daraja eneo hilo kungehitaji zaidi ya shilingi bilioni ambapo katika kipindi  hicho hawakuwa nazo fedha hizo. Diwani wa Kata ya Pangani, BW.AGUSTINO MDACHI amewataka wananchi ...

VIDEO-WAUUGUZI WAPONGEZWA KWA KUJITOA KUSAIDIA WAGONJWA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/05/2016 11:34:06 Wauguzi nchini wamepongezwa kutokana na mchango wao wanaoutoa kwa binadamu wenzao wanapokabiliwa na magonjwa mbalimbali. Mbunge wa Kibaha mjini, Mh. SLYVESTER KOKA amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo yamefanyika katika Hospitali teule ya rufaa ya Mkoa ya Tumbi. Ambapo amesema muuguzi hana tofauti na Mama linapokuja kwenye suala la malezi ya mgonjwa, ametoa mfano  mtoto anapokuwa amejichafua aidha kwa kujikojolea au kujinyea ni aghalabu Baba kumchukua na kumbeba mpaka pale mama atakapomsafisha. Mbunge huyo BW. KOKA amefananisha hali hiyo na mgonjwa anapokuwa hawezi kufanya lolote na kujisaidia mahali halipo ni muuguzi ndiye anayekuwa karibu naye bila kujali kama ni ndugu au la. Naye Kaimu muuguzi mkuu wa Hospital ya Tumbi, BW. DAVID WAWA amesema kuwa siku ya wauguzi duniani ni maalum kwa ajili ya kukumbushana wajibu wao ikiwa pamoja na kula kiapo kipya ili kusaidia kutekeleza majukumu...

VIDEO-UTALII WA NDANI WAHIMIZWA

Image
Ben Komba/Pwani/Tanzania/12/05/2016 10:49:28 Katika kuhamasisha utalii wa ndani umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi hivi karibuni kimefanya ziara katika mbuga za wanyama  Mikumi ili kuunga mkono mkakati wa serikali katika kuwahamasisha wazawa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliambatana na msafara huo, Mwenyekiti wa UVCCM mjini Kibaha, BW. IDD KANYALU amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii ndani na kuongeza kipato kwa Taifa. BW.KANYALU amebainisha mbali ya lengo kuu hilo pia ni pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi wa umoja wa vijana wa CCM mjini Kibaha kwa kuwawezesha kuwaweka pamoja na kutafakari mambo mbalimbali yta kukimarisha chama. Mhifadhi wa Mbuga ya wanyama wa Mikumi BW. ABDALLAH CHOMA amewaambia watalii hao wa ndani kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha ...

UVCCM KIBAHA MJINI YAHIMIZA UTALII WA NDANI

Ben Komba/Pwani/Tanzania/12/05/2016 10:49:28 Katika kuhamasisha utalii wa ndani umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi hivi karibuni kimefanya ziara katika mbuga za wanyama  Mikumi ili kuunga mkono mkakati wa serikali katika kuwahamasisha wazawa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliambatana na msafara huo, Mwenyekiti wa UVCCM mjini Kibaha, BW. IDD KANYALU amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii ndani na kuongeza kipato kwa Taifa. BW.KANYALU amebainisha mbali ya lengo kuu hilo pia ni pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi wa umoja wa vijana wa CCM mjini Kibaha kwa kuwawezesha kuwaweka pamoja na kutafakari mambo mbalimbali yta kukimarisha chama. Mhifadhi wa Mbuga ya wanyama wa Mikumi BW. ABDALLAH CHOMA amewaambia watalii hao wa ndani kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha mb...

VIDEO-MAHAKAMA YALALAMIKIWA KUPOTOSHA HUKUMU KISARAWE

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/05/2016 14:49:31 Katika hali ya kushangaza mahakama ya wilaya ya Kisarawe imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja cha nje, Mtuhumiwa PETRO GEMBE kwa kosa la uvamizi na ubakaji iliyokuwa inamkabili akishtakiwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.  Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo mwandishi wa habari hizi ameipata, Inadaiwa tarehe 24 Juni mwaka 2015 mtuhumiwaPETRO GEMBE akiambatana na wenzie majira ya saa moja usiku walivamia makazi ya BW.FESTO LOYA kwa nia ovu. Inasemekana mtuhumiwa huyo na wenzie walipora mifugo ng”ombe 53 na wenye thamani 21,000,000/=  na fedha taslimu shilingi milioni 48,350,000/= ambapo vitu vyote vilivyoporwa vina thamani ya shilingi milioni 69,350,000/=  mali ya BW. FESTO LOYA ikiwa pamoja na kuondoka na mkewe DANGA’U GEIDA na kuishi naye kama mke bila idhini yake. BW.LOYA amebainisha akiwa mkazi wa kijiji cha Kimalamisale amesikitishwa na hukumu hiyo iliyotolewa na hakimu mkazi  wa mahakama ya w...

MAHAKAMA YALALAMIKIWA KUPOTOSHA HUKUMU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/05/2016 14:49:31 Katika hali ya kushangaza mahakama ya wilaya ya Kisarawe imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja cha nje, Mtuhumiwa PETRO GEMBE kwa kosa la uvamizi na ubakaji iliyokuwa inamkabili akishtakiwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.  Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo mwandishi wa habari hizi ameipata, Inadaiwa tarehe 24 Juni mwaka 2015 mtuhumiwaPETRO GEMBE akiambatana na wenzie majira ya saa moja usiku walivamia makazi ya BW.FESTO LOYA kwa nia ovu. Inasemekana mtuhumiwa huyo na wenzie walipora mifugo ng”ombe 53 na wenye thamani 21,000,000/=  na fedha taslimu shilingi milioni 48,350,000/= ambapo vitu vyote vilivyoporwa vina thamani ya shilingi milioni 69,350,000/=  mali ya BW. FESTO LOYA ikiwa pamoja na kuondoka na mkewe DANGA’U GEIDA na kuishi naye kama mke bila idhini yake. BW.LOYA amebainisha akiwa mkazi wa kijiji cha Kimalamisale amesikitishwa na hukumu hiyo iliyotolewa na hakimu mkazi  wa mahakama ya wil...